Kuzaliana kunamsaidia nini kiumbe anayezaa?

Kuzaliana kunamsaidia nini kiumbe anayezaa?

Tunazaana kwasababu tunakufa.Aliyeumba viumbe hai vinavyokufa aliweka uzao ndani ya hivyo viumbe.Kwahiyo kufa ndiko kunakoongoza uzao ulioko ndani ya viumbe hai.Kwahiyo viumbe wanaokufa wanapambana wasitoweke kwenye uso wa dunia kwakuakikisha wanazaana.Ni vita kati ya kifo na uzazi.Na hilo ni jambo la asili ambalo binadamu pamoja nakujaribu kuliingilia bado hataweza kulikomesha kwasababu akikomesha kuzaa maana yake kifo kitakua kimeshinda na matokeo yake binadamu atatoweka duniani.Kama kungekua hakuna kufa pia kungekua hakuna kuzaana.Tungeumbwa wengi alafu tukaishi tu.ila waliumbwa wachache wakawekewa kifo na uzazi ili iwe ni vita kati ya kuwepo au kupotea.Kwahiyo kuzaa kuna maana kubwa sana kiuzao kuliko faida ya binadamu mmoja mmoja.
 
Yani maisha niyaishi mimi alafu nisitake faida niipatayo katika maisha? Sasa si angekuja huyo Mungu kuishi akaachana na mimi [emoji848]
Kwani unajijua kuwa wewe ni nani? Wewe sio huo mwili wako, wala wewe sio hilo jina lako.


YESU NI KRISTO
 
Nimekuwa najiuliza sana hili swali. Nakumbuka mara ya kwanza kuwaza hivi nilimuuliza mama. Nikasema sisi lengo letu nini? Bibi kamzaa mama, bibi anazeeka anakufa. Na mama anatuzaa sisi, nae atazeeka na atakufa vile vile. Na mimi naanza kupambana na mihangaiko ya maisha kisha nazaa watoto. Then what?


Kama mleta maada alivyosema, labda kama tungekuwa hatufi ingeleta maana.
Kama watu wa BC hakuna wanachofaidika na kizazi hiki ya nini kuzaana? Si tustop biashara kichaa iishie hapa?

au sisi tumefungwa na kitu fulani ambacho lengo lake ni kitoweo. Kama vile sisi tunavyofuga kuku.

Inafikilisha kwa kweli forget wandugu.
Haahhaaaah! Eti tumefugwa. Umefikiri mbali sana japo hoja yako inafikirisha sana. Lakini ingekuwa na sisi ni kitoweo obviously tungeona
 
Nimekuwa najiuliza sana hili swali. Nakumbuka mara ya kwanza kuwaza hivi nilimuuliza mama. Nikasema sisi lengo letu nini? Bibi kamzaa mama, bibi anazeeka anakufa. Na mama anatuzaa sisi, nae atazeeka na atakufa vile vile. Na mimi naanza kupambana na mihangaiko ya maisha kisha nazaa watoto. Then what?


Kama mleta maada alivyosema, labda kama tungekuwa hatufi ingeleta maana.
Kama watu wa BC hakuna wanachofaidika na kizazi hiki ya nini kuzaana? Si tustop biashara kichaa iishie hapa?

au sisi tumefungwa na kitu fulani ambacho lengo lake ni kitoweo. Kama vile sisi tunavyofuga kuku.

Inafikilisha kwa kweli forget wandugu.
Tobaa. Hapo kwenye kitoweo [emoji22][emoji22][emoji22]
Sijui mie nafugwa na nani saa!!!?
 
Mwili wa binadamu na viumbe wengine wote unahangaika sana na mambo mawili. Kusurvive na kuzaliana. Sasa najiuliza kuzaliana kunamsaidia nini kiumbe anayezaa. Kuendeleza kizazi cha ng'ombe, kunamsaidia nini ng'ombe anayezaa. Binadamu walioishi miaka ya BC huko, wanafaidika vipi na kuendeleza uzao wa binadamu? Kungekuwa hamna kufa ningeweza kidogo kuelewa.

Zaidi naona uzazi unamnyonya mzazi kiafya, kichumi nk. Kuzaliana kunamsaidia nini anayezaa?
Mtafute 'designer' wa binadamu na viumbe vingine vyote akupe jibu, kwani huyo ndio haswa mwenye jibu sahihi.
 
Upo sahihi coz ni kama betting unaweza zaa mtoto na akaja kuwa liability.

But why kunakiwa na upendo kati ya mzazi na mtoto.?
Hamjamuelewa mwamba, hazungumzii short term profit anazungumzia longterm.babu wa babu wako wa babu wako amefaidika na nn kuhusu wewe.ukifikilia kwa umakini unaona hafaidiki na chochote.
Sasa swali lina pop up! Kichwani mwake kua au tunaishi .na hatujui kua labda sisi nikitoeo.kua ukifa unaenda kuliwa chakula kama mboga?

Fikilia viumbe vingine vyote vinaishi kwa faida ya mwanadamu.vina survive vina zaliana kuhakikisha tu mwanadamu anaishi vizuli,anapata cha kula kingi.mimea ikihakikisha mvua na hali ya hewa safi .ingawa yenyew haijui kua inatufaudisha. Kama sisi ambavyo hatujui last consumer wetu ni nani?

Sema mda ukiipima kwenye dini haina mashiko kivile maana inajibika kirahisi sana kupitia maandiko.

Ila ukiifikilia kama jamaa mmoja iv humu nimemsahau jina .anasema kua sisi tuliubwa kwa kazi maalumu ya kuchimba dhahabu duniani na viumbe flani hiv vinavyopatikana angaa za mbali.mbingu ya 7ukoo.na tukabakishwa kama vitoeo ,kama ilivyo kwa wasukuma ambavyo wanafunga ng'ombe kwa ajili ya chakula na kuwasaidia kazi za kubeba mizigo na kulima.
Kua wasela wanakuja wanajichagulia mwanadamu mmoja mmoja wanatafuna.ili tusiwashitukie wakatupa maandiko ya dini ili tuongozane bila vurugu.😂
Ukifaa kwa ugonjwa nahisi ww wanakutupa wanawapa mbwa zao maana ww nisawa sawa na kuku aliekufa kwa kideli wasela hawali vibudu.
Mawindo yao nikupitia ajali, majanga yamoto na mengine ya kutatanisha
 
Mada fikirishi sana hii.. Iko hivi, ili uzae/ uzalishe mwanadamu unalazimika kupeleka/kupelekewa moto, kitu kitakachofanya upate utamu wa ajabu sana, hiyo ndiyo faida pekee![emoji39][emoji2957].
 
Back
Top Bottom