Kuzibua njia ya ABS Module

Kuzibua njia ya ABS Module

Extrovert

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2016
Posts
70,785
Reaction score
186,690
Baada ya kula buyu siku sio nyingi nilifuatilia chanzo na kugundua ABS module imeziba kwenye njia moja na kupelekea gari kutopeleka hydraulic kwenye mguu wa kushoto mbele. Hivyo ililock brakes upande mmoja na hatimae gari ikapiga u turn ya maana.

Je, naomba kujua kwamba hiki kidude kinaweza kufanyiwa repair kwa maana kuzibua njia ilioziba ama ntatakiwa ninunue kingine tu? Kuna signal kuwa ABS ina shida inaonesha kwenye dashboard lights.
images.jpeg
 
Yes, hicho kidude kinaweza kufanyiwa repair..la kama kimeharibika hakirekebishiki unanunua kingine na kukireplace. Nilinunua 120,000(used from JP) pamoja na kufungiwa na kuanzia hapo sijawahi pata tatizo.
 
Kwanini uhangaike na repair kwa gari ya Mjapani..!! Tandale spares za Wajapani kama zote na bei chini.. Tofauti na Wajerumani mpaka uagize wiki 4..!
 
Bado tatizo sio kuziba pekee, Abs zina fail safe procedures , check and balance , ndo mana kila mguu una sensor,
Procedure ya kwanza kabisa ni anti lock , hii inafanywa na sensor , tairi lisilozunguka maana yake ni kuwa halitakiwi kupata brake force.

Kwamba ulikanyaga breki halafu hydraulic solenoid ikashindwa ku release pressure kutokana na kuziba ? Hilo haliwezi kutokea , maelezo yake ni marefu sana , ila najua haiwezekani.

Chances kwa scenario yako
1, inawezekana rotor ilishindwa ku regulate pressure precisely.

2, kuna uwezekano kulifanyika modification kwenye pipes hasa zile flexible za miguuni.

3.Abs motor that rotates rotor,asks fo a lot of current during its operation, kama uliwahi kupeleka gari uchochoroni fundi akachezea waya kuna uwezekano pia motor haikuoperate efficienty ,ni kama vile uwashe gari wakati battery terminals zipo loose .
 
Bado tatizo sio kuziba pekee, Abs zina fail safe procedures , check and balance , ndo mana kila mguu una sensor,
Procedure ya kwanza kabisa ni anti lock...
Mods hazijafanyika mkuu zaidi nilibadili brake master cylinder nikafunga mpya. Ila still mguu wa kushoto hausagi ile rotor disc ina kutu while ya kulia unasaga fresh imekuwa silver kabisa.

Kufuatilia ikaonekana pressure ya hydraulic ni ndogo toka kwenye pipe yake kumbe shida ni hiko kidubwana hakitoi wese kwa pressure kama njia nyingine.
 
Baada ya kula buyu siku sio nyingi nilifuatilia chanzo na kugundua ABS module imeziba kwenye njia moja na kupelekea gari kutopeleka hydraulic kwenye mguu wa kushoto mbele. Hivyo ililock brakes upande mmoja na hatimae gari ikapiga u turn ya maana.

Je, naomba kujua kwamba hiki kidude kinaweza kufanyiwa repair kwa maana kuzibua njia ilioziba ama ntatakiwa ninunue kingine tu? Kuna signal kuwa ABS ina shida inaonesha kwenye dashboard lights. View attachment 2419960
Guys, Don't mess up with ABS.

Nimewahi andika humu ndani. Gari ikiwa na fault yoyote ya ABS inakuwa inafanya kazi katika Non-ABS mode.

1. ABS inakusaidia matairi yasilock wakati wa kufunga brake. Tairi zikilock huwezi hata kukata kona.

2. ABS inakupa very short braking distance.

3. ABS inakupa stability wakati wa hard braking. Kuna mazingira mfano hasa barabara za vumbi. Hard braking inafanya gari inashake sana, unaweza hata kula mzinga. Hii imemtokea jamaa yangu.

4. ABS inakupa very good steering experience hasa wakati wa braking.

5. ABS inakupa good driving experience kwenye utelezi.

Tafadhali angalia video hii labda unaweza kuelewa ABS ina umuhimu gani kwenye gari yako.



Kwako mtoa maada, ABS modules nyingi ni irreparable. Tafuta ABS module nyingine funga.
 
Kipindi nipo na Carina ti ilisumbua Sana hilo dude Hadi nilibadilisha kama vipi ni Bora ununue module nyingine Tu kuliko kuanza kurekebisha
 
Najua ABS Ni Nini, umuhimu wake na all staffs lkn Nilishaendesha Gari taa ya ABS ikiwa ON kwa zaidi ya miaka 3 Na ikipiga kazi fresh kabisa mpk nikaiuza hio gari.

Nb: usalama kwanza
 
Back
Top Bottom