Kuzuia mashabiki kuingia uwanjani, Mwafrika ana tatizo la kufikiri

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Kwa ufupi sana,

CAF imezuia mashabiki wa Simba SC na timu zingine huko Afrika wasiingize mashabiki uwanjani. Lakini kidogo kidogo unasikia nchi zingine zimeruhusiwa ziingize idadi fulani. Nimesoma Al Hilal na Nkana wameruhusiwa idadi fulani.

Unajiuliza hivi sisi ngozi nyeusi tunatumia akili gani? Kwanini nchi zingine ziruhusiwe zingine zisiruhusiwe? Wametumia vigezo gani?
Taarifa zinaonyesha wanachama wengine wanaomba. Kwa hiyo hakuna standards badala yake mwanachama anaomba. Huu ni undezi. Hawaoni kama wanaleta vurugu?

Nini maana ya standards? Standards au viwango huwekwa na bodi mbalimbali kwa ajili ya harmonization na kuepuka mikanganyiko. Standards zinatakiwa zitumike na kila mwana bodi. Kama standards ni kutokuingiza mashabiki basi ilitakiwa ibaki hivyo, na kama ni kuingiza kiasi fulani basi ingebaki hivyo kwa wanachama wote. Unapolegeza masharti kwa baadhi ya wanachama unaleta mianya ya rushwa na upendeleo.

Nashangaaa Simba na TFF kwa nini wamechukulia poa jambo hili. Ama ni ile dhana ya nidhamu ya uoga au nao ni sehemu ya tatizo. Mnakubalije tusiingie uwanjani wakati controls za nchi dhidi ya Corona ni relaxed watu wanaendelea na shughuli zao?

Nasema tena, Afrika bado tuna safari ndefu ya kuimarisha taasisi zetu.
 
Hii imekuja baada ya uongozi mpya wa CAF kuingia Madarakani hivyo tutegemee kuona Vituko vingi.

Pia TFF na Simba wamelegea sana juu ya hili swala. Lakini pia nyuma ya panzia yawezekana kuna Kafitna kamefanyika maana mafanikio ya simba yanawakera wengi.
 
Kwenye kundi letu nafikiri tumeathiriwa na Al Ahly hii team ina sauti sana CAF.

Kimahesabu al ahly anaweza toka makundi safari hii. Kama kesho anapigwa na vita. Then sisi tushinde. Halafu yeye akitufunga kwao anakuwa na point 7. Wakati huo vita nae kamfunga msudani point 10.
Then game ya mwisho sisi na vita point kumi wote hata tukitoka sare mwarabu anakuwa katoka🤣 maana sisi na vita tutakuwa na point 11. Yeye al ahly point 10.
 
Sisi kama mashabiki wa yanga hiyo ni furaha kwe2 [emoji3517]
 
Acheni kulaumu CAF bila sababu za msingi. Mechi ya Simba na Al Ahly, kuna idadi kadhaa ya mashabiki waliruhusiwa, ila kutokana na kutopenda kufuata utaratibu, idadi ilikiukwa, wakaingia washabiki wengi zaidi.

Hii ndio imepelekea uhamuzi huu.
 
Acheni kulaumu CAF bila sababu za msingi. Mechi ya Simba na Al Ahly, kuna idadi kadhaa ya mashabiki waliruhusiwa, ila kutokana na kutopenda kufuata utaratibu, idadi ilikiukwa, wakaingia washabiki wengi zaidi.

Hii ndio imepelekea uhamuzi huu.
Umegonga kwenye point.

Social distancing haikuzingatiwa. WaTz tusiwe watu wa kulalama bila kufikiri.
 
pia Covid ipo bongo kwann wasizuie mikusanyiko isiyo na lazima . Nawaza tu kwa sauti
 
Acheni kulaumu CAF bila sababu za msingi. Mechi ya Simba na Al Ahly, kuna idadi kadhaa ya mashabiki waliruhusiwa, ila kutokana na kutopenda kufuata utaratibu, idadi ilikiukwa, wakaingia washabiki wengi zaidi.

Hii ndio imepelekea uhamuzi huu.
Hii sababu yako ya kuokota umeiokotea wapi?

Hao CAF walisema lini hiyo sababu?
 
vipi kuhusu zile points z’zetu’ 3 za mezani kutoka kwa al mereikh ??? Naanza kuhisi hawa CAF ni wananchi hawa!
 
Wakati ukilalamika hilo, fikiria mechi ya Simba dhidi ya Plateau, platinum, na Al Ahly ambazo zote hizo Simba wamecheza na kujaza washabiki uwanjani wakati timu pinzani zimecheza pasipo na washabiki dhidi ya Simba (plateau United, platinum fc na As Vita)
 
Acheni kulaumu CAF bila sababu za msingi. Mechi ya Simba na Al Ahly, kuna idadi kadhaa ya mashabiki waliruhusiwa, ila kutokana na kutopenda kufuata utaratibu, idadi ilikiukwa, wakaingia washabiki wengi zaidi.

Hii ndio imepelekea uhamuzi huu.
Nilihisi hii adhabu kutokea ingeepukwa kama walioingia wangekaa mbalimbali ila sasa jinsi walivyokaa haikuwa na maana
 
vipi kuhusu zile points z’zetu’ 3 za mezani kutoka kwa al mereikh ??? Naanza kuhisi hawa CAF ni wananchi hawa!
Simba haikuomba kupewa point za mezani, na pengine hata haizihitaji. Simba waliomba wapewe ufafanuzi kuhusu uhalali wa hao wachezaji kuichezea Al Merrikh, na pengine ombi lao linaweza kuwasaidia katika mechi hii inayokuja (maana Al Merrikh wanaweza wakasita kuwapanga) na zaidi litawasaidia Al Hilal wanayogombania wachezaji hao
 
Imekuwaje tena. Wakati nyie nyie kila siku kule siasani mlikuwa mnataka serikali itowe tamko kuhusu ugonjwa wa kupumua.

Nadhani CAF imewasaidia ,hivyo acheni ulalamishi nyie chezeni mpira. Teh
 
CAF hii mpya ni ya kipuuzi sana

Kwann baadhi ya timu ziruhusiwe mashabiki????

Hii CAF inataka kudidimiza mpira wetu.
 
Na tumeshajibiwa na CAF kwamba wale wachezaji walifungiwa kwa mechi za ndani tu kwahiyo walikua na haki kucheza mechi na Simba. Kwa mujibu wa Barbara leo
 
Hii sababu yako ya kuokota umeiokotea wapi?

Hao CAF walisema lini hiyo sababu?
Huwa sijadiliani na watu wanaojiandaa kubisha ilhali hawana taarifa za kutosha au taarifa sahihi.

Endelea kushikilia sababu uliyonayo mkuu
 
Unaongea kama shabiki wa Simba au kama mwanamichezo?
Jibu lipo wazi, ameongea kama mshangiliaji wa simba. Maana shabiki wa kweli angekuwa na taarifa sahihi za timu, na endapo angekuwa mwanamichezo, basi angekuwa anaweza kupokea taarifa asizozijua vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…