Kuzuia mchanga wa dhahabu, Magufuli anastahili pongezi. Tusiishie kwenye madini tu, na gesi je?

Kuzuia mchanga wa dhahabu, Magufuli anastahili pongezi. Tusiishie kwenye madini tu, na gesi je?

Wanabodi
Kwenye mazuri tupongeze, mabaya tukosoe na panapostahili ushauri au angalizo tutoe.

Miongoni mwa vitu vizuri rais Magufuli alivyovitaja ni kujiapiza kuwa mchanga huo hautoki, hata kama tunashindwa kuusafisha mchanga huo, then ikibidi hata hiyo migodi ifungwe na ifungwe tuu mpaka Tanzania tupate uwezo wa kuuyeyusha huo mchanga.

Huu ni uzalendo wa hali ya juu sana. Mwingine aliyefanya hivi ni Mwalimu Nyerere, alizuia kabisa kuchimbwa madini mpaka tupate uwezo wa ndani wa kuyachimba, bahati mbaya Nyerere alipoondoka na kuingia Mwinyi, akatoa rukhsa kuchimbwa kwa dhahabu yetu na kiukweli tumeishia kuibiwa kwa kupata just a peanut huku wenye migodi wakikomba kila kitu na kuishia na faida yote huku wakituachia mashimo! .

Mambo mengine jameni sio tunashangilia tuu kisha baadae tunakuja kurudi kule kule!. Hili la mchanga nawaomba wenye kumbukumbu wekeni kumbukumbu sahihi ya bandiko hili kuwa tutabana wee lakini mwisho wa siku tutaachia tena tukiwa tumeumizwa katokana na kubana. Ili tusiumizwe, Tanzania lazima haya makontena 277 tuliyoyakamata, lazima tuyasimamie wenyewe, yachenjuliwe ili tujue kilichomo, hivyo kuweza ku calculate kiasi walichokuwa wanatuibia. Majadiliano yoyote bila udhibitisho wa kilichomo, tutapigwa tena, na mchanga utaendelea kuchenjuliwa kule kule unakochenjuliwa!. ili tusijue kilichomo kwenye mchanga huu, wanyonyaji hawa, watakuwa tayari kufanya lolote, hata ikibidi kutulambisha asali, watatulambisha, lakini mchanga uondoke!.

Kuna vitu kuvifanya kunahitaji tuu nia ya dhati, na kuna vitu kuvifanya kunahitaji sio tuu nia ya dhati, bali pia uwezo. the capacity na ruhusa ya wakubwa wa dunia hii, ndipo uvifanye.

Paskali
Nafanya mapitio niliwahi kushauri nini, na sasa kinatokea nini, haya wajameni, mkataba umesainiwa, makinikia yanaondoka
Naitafuta ile clip ya mtu alijiapiza kuwa sasa mchanga hautoki!.
P
 
Back
Top Bottom