Kuzuiwa kwa fomu 2c: Mapato ya mauzo ya dawa Muhimbili yaongezeka hadi billioni 14

Kuzuiwa kwa fomu 2c: Mapato ya mauzo ya dawa Muhimbili yaongezeka hadi billioni 14

Peter Madukwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2012
Posts
3,139
Reaction score
2,488
Kufuatia serikali kupitia wizara ya afya kuzuia matumizi ya fomu ya dawa namba 2C ya NHIF; Kwa mujibu wa waziri wa afya, mapato ya dawa ktk hospitali ya Taifa Muhimbili yameongezeka kutoka wastani wa billion 2-4 kwa mwaka hadi kufikia wastani wa billioni 10-14.

Fomu 2C ya mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) ilikuwa inatumika kuchukulia dawa ktk maduka pale ambapo inaonekana dawa hakuna ktk kituo cha kutolea huduma ya afya.

Kwa mujibu wa agizo la wizara ya afya; lengo la wizara ya afya kusitisha matumizi ya fomu 2C ilikuwa kuhakikisha kuwa watendaji wa vituo vya kutolea huduma ya afya wanawajibika ktk kuhakikisha kuwa dawa zote zinapatikana muda wote ktk hospitali, vituo vya afya na zahanati badala ya kutegemea maduka binafsi.

Hongera kwa serikali ya awamu ya sita kwa hatua hizi madhubuti; kimsingi matumizi ya fomu namba 2C yalichangia kiasi kikubwa kuhujumiwa kwa tatizo la dawa ktk vituo vya kutolea huduma.

Mungu ibariki Tanzania.
IMG-20220705-WA0002.jpg
 
Huu ni uwendawazimu wa wazi kabisa.
Samahani naomba kuuliza.
Muhimbili zoezi la kuzuia fomu namba 2c lilianza mwaka juzi au mwaka Jana?
Maana kwenye vituo vya afya huku tangu zoezi lianze hata wiki haijatimia.
Viongozi wetu ni wezi lakini wanaogopa sana kuibuwa
 
Hii ni kuwakomoa client, ni ngumu kwa kituo kuwa na kila aina ya dawa kwa nyakati zote, ikizingatiwa kuwa MSD hawezi leta dawa kila wiki.

Hapo tujipange kufuata dawa duka la nje tena kwa CASH.
 
Tushangae wote mana hii habari nimeisikia sidhani hata wiki kama imeisha.
Hawa watu sijui wanatuchukuliaje.
 
Mleta uzi wewe ni chawa halafu mjinga..tuambie hizo fomu zilizanza kuzuiwa lini?

Kuweni basi na akili yani imefikia hatua hadi vilaza sikuhizi ndio mana waweka waeneze propaganda?

#MaendeleoHayanaChama
 
Jmabo la msingi ahakikishe dawa zinapatikana kwenye hospitali na vituo vya afya hizo B'S hazituhusu kiviiiiiile
 
Kwahiyo Zoezi lilianzia Muhimbili miaka kadhaa nyuma kwa majaribio ndio likaleta mafanikio hayo au mshazoea kutuona watoto?
 
Upotoshaji mkubwa huu. Kwanza hospitali nyingi hazina dawa husika. Mfano wagonjwa wa kisukari kuna baadhi ya dawa hazipo pamoja na gluco test strips hakuna unaambiwa ukanunue. Wenye pesa za kununua na kumudu gharama ni wachache. Wengi wataishia kukaa bila kutumia dawa kitu ambacho ni hatari kwa maisha.
 
Mleta uzi wewe ni chawa halafu mjinga..tuambie hizo fomu zilizanza kuzuiwa lini?

Kuweni basi na akili yani imefikia hatua hadi vilaza sikuhizi ndio mana waweka waeneze propaganda?

#MaendeleoHayanaChama
Ni kweli hazitumiki tena wala siyo uongo. Nilienda hospitali nikaambie thyroxine hakuna na hakuna cha fomu ya bima nikanunue hizo dawa cash dozi 40, 0000/- kama huna hiyo hela utajua mwenyewe.
 
Hii ni kuwakomoa client, ni ngumu kwa kituo kuwa na kila aina ya dawa kwa nyakati zote, ikizingatiwa kuwa MSD hawezi leta dawa kila wiki.

Hapo tujipange kufuata dawa duka la nje tena kwa CASH.
Kituo kina wajibu wa kuhakikisha dawa zinapatikana; kama hakiwezi maana yake hakina sifa
 
Jmabo la msingi ahakikishe dawa zinapatikana kwenye hospitali na vituo vya afya hizo B'S hazituhusu kiviiiiiile
Hiyo ndiyo target ya serikali na ndiyo maana Mh Waziri amewataka watendaji kuhakikisha dawa zinapatikana muda wote
 
Upotoshaji mkubwa huu. Kwanza hospitali nyingi hazina dawa husika. Mfano wagonjwa wa kisukari kuna baadhi ya dawa hazipo pamoja na gluco test strips hakuna unaambiwa ukanunue. Wenye pesa za kununua na kumudu gharama ni wachache. Wengi wataishia kukaa bila kutumia dawa kitu ambacho ni hatari kwa maisha.
Ni wajibu wa vituo vya kutolea huduma kuhakikisha dawa zinapatikana badala ya mgonjwa kutafuta dawa madukani
 
Nadhani wamefanya extrapolation!! Kama kwa wiki moja tumepata kiasi hiki, je kwa wiki zote za mwaka tutapata sh ngapi? Hapo unafanya hesabu ya cross-multiplication na kupata jibu!! Hiyo ni kawaida kabisa!!
 
Back
Top Bottom