Kuzuiwa kwa fomu 2c: Mapato ya mauzo ya dawa Muhimbili yaongezeka hadi billioni 14

Kuzuiwa kwa fomu 2c: Mapato ya mauzo ya dawa Muhimbili yaongezeka hadi billioni 14

Kituo kina wajibu wa kuhakikisha dawa zinapatikana; kama hakiwezi maana yake hakina sifa
Kituo kina wajibu wa kuhakikisha dawa zinapatikana; kama hakiwezi maana yake hakina sifa
Wapite kugagua kama watakuta hizo dawa. Yani mateso kwa wasio na uwezo wa kununua cash. Vitu kama gluco taste strip za wagonjwa wa kisukari ni elfu hamsini kwa strips 25 sidhani wote tuna uwezo wa kununua.
 
Kufuatia serikali kupitia wizara ya afya kuzuia matumizi ya fomu ya dawa namba 2C ya NHIF; Kwa mujibu wa waziri wa afya, mapato ya dawa ktk hospitali ya Taifa Muhimbili yameongezeka kutoka wastani wa billion 2-4 kwa mwaka hadi kufikia wastani wa billioni 10-14.

Fomu 2C ya mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) ilikuwa inatumika kuchukulia dawa ktk maduka pale ambapo inaonekana dawa hakuna ktk kituo cha kutolea huduma ya afya.

Kwa mujibu wa agizo la wizara ya afya; lengo la wizara ya afya kusitisha matumizi ya fomu 2C ilikuwa kuhakikisha kuwa watendaji wa vituo vya kutolea huduma ya afya wanawajibika ktk kuhakikisha kuwa dawa zote zinapatikana muda wote ktk hospitali, vituo vya afya na zahanati badala ya kutegemea maduka binafsi.

Hongera kwa serikali ya awamu ya sita kwa hatua hizi madhubuti; kimsingi matumizi ya fomu namba 2C yalichangia kiasi kikubwa kuhujumiwa kwa tatizo la dawa ktk vituo vya kutolea huduma.

Mungu ibariki Tanzania.
View attachment 2281464
Mnh hawatoi form 2c ni mda sana
 
Back
Top Bottom