Kwa aina ya Wachambuzi tulionao tunawahitaji kina Haji Manara wengi

Kwa aina ya Wachambuzi tulionao tunawahitaji kina Haji Manara wengi

Naanza kwa Kusema 'BIG UP' Kwa Manara.Kwa Kueleza Waziwazi bila Woga Kitendo kibaya Mno Kilichofanywa na Yanga,Kukimbia Mechi Ya Darby bila kujali Umati Ule uliojazana Pale Kwa Kivuli cha Kanuni.La Pili ambalo nalo linastahili pongezi ni kuonyesha Uzandiki kwa Wanaojiita wachambuzi...kwa kutetea na kuubeba Utopolo Uliofanywa na Utopolo Yenyewe 'eti wamefanya Kitendo Cha kishujaa.Hawa Utopolo hawana pa Kuchoropoka mwaka huu, Naziona game mbili clear zinakuja, ya FA na Hii ya VPL ambayo itapangiwa tarehe nyingine .Lazima Vyura wapigwe...!
Wachambuzi Uchwara wamekuwa wengi mno....! Tatizo la ajira linakuja na matokea anuai, wengine Wanavamia fani...!
Upumbafu haujaisha tu
 
Naunga mkono hoja ya Haji. Huwezi kuacha kucheza mpira baada ya game kusogezwa mbele kwa masaa

Huu si uungwana hata kidogo ambao wametendewa mashabiki na wadau wa soka kwa vile kuna games nyuma zimefanywa hivyo, kanuni ilikuwa wapi? Au kanuni kwa Simba na Yanga tu..!
Wapumbafu mpo wengi
 
Kwenye matamko ya serikali hayaanzii kwenye kwanini waliahirisha bali way forward kwenye swala la mechi itachezwa lini. Ndio utajua TFF walipewa maagizo.

Yanga wanaivimbia serikali wakihisi wanaivimbia TFF.
Tff walipaswa kuambatanisha na barua ya wizara ya kupeleka mbele mchezo

Yanga wako sahihi mara [emoji817]
 
Nikimsikia mchambuzi mmoja anaitwa dada ni taka taka kabisa.

Anasema Simba imenufaika na corona ndiyo maana imefika hapo ilipo!Ni ajabu sana kwani Simba siyo mara ya kwanza kifika hapo.
Lakini pia wamewahi kufika fainali za CAF.

Kusema wamefaidika na corona ni dharau za wazi kwa uwekezaji uliofanyika,kwa wachezaji wa Simba,na kwamba anawaona si lolote isipokuwa ni corona imewabeba.
Kibaya sana ni pale hajui hata kuwa ligi ya Misri haikusimama na bado tumewafunga Al ahly.
Simba imeshinda mechi za ugenini na si nyumbani tu.

Wanatia kinyaa kwa uchambuzi wao usio fair ila unajali matumbo yao tu,hasa kwa vile wanaambiwa wafikiri nini na anayewalipa
Mtu akikuambia korona imeibeba Simba mwambie mbona NAMUNGO haikumbeba?

Halafu mwambie ABAKI NA UJINGA WAKE.
 
Ww mwenyew umeandika kwa mihemko kwahy ulitaka wandishi wapindishe ukwel
 
Haji Manara asipewe nafasi ya kuzungumza kwenye mambo wanayo hitaji matumizi ya akili yeye awe mwamasishaji. Kama klabu yake itaendelea kumtumia inatakiwa ijuwe uwezo wake kwenye mambo rahisirahisi, Mambo wanayo hitaji akili atafutwe wa kuzungumza la sivyo kunasiku ataleta tabu kwa klabu yake.
 
Manara Kajenga Hoja Yenye mashiko Mechi kusogezwa mbele masaa mawili haimaanishi mchezo umehairishwa...Sasa Wachambuzi wanaacha hoja Wanasifia Ushujaa Wa Yanga 'kutimua mbio' .
All in all Ipo haja na Wao kujitathmini wasitumie vyombo vyao Vibsya.
Mabadiliko hayo ni kinyume cha kanuni ya 15(10) za Ligi Kuu
inayohusu taratibu za michezo ambayo unasema mabadiliko yoyote ya muda wa kuanza Yatajulishwa ipaaavyo kwa pande zote mbili husika za mchezo angalau masaa 24 kabla ya muda wa awali.


Hiyo kanuni inaongelea kuahirisha au mabadiliko?!

Nikimtag Aden Rage nitakuwa nakosea?!
 
Back
Top Bottom