Kwa ajili ya kumbukumbu: Magufuli hatojiongezea muda

Kwa ajili ya kumbukumbu: Magufuli hatojiongezea muda

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Ok, so, me being me. The independent minded guy that I am. Native citizen of Realville. That straight shooter that I am. I am no shrinking violet when it comes to expressing my views.

So I’m going to go out on a limb today and say it. If this means I’ll have to eat crow a couple years from now for being dead wrong, then so be it.

Ni hivi: Rais Magufuli [sidhani] kama atajiongezea muda ili atawale kwa zaidi ya miaka 10.

Minong’ono na hofu iliyopo hivi sasa kwamba atajiongezea muda, ni maneno tu. Ni hewa.

Kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu zifuatazo:

1. Urais ni mzigo. Ni mzigo mzito wenye kuleta msongo wa mawazo. Ni aina ya mateso flani hivi.

Kwa mtu anayejali kufanya kazi na siyo kula bata, basi mtu wa aina hiyo hawezi kutamani kuwepo madarakani kwa kipindi kirefu kuzidi miaka 10.

Ila kwa mtu mla bata asiyejali kazi, kama alivyokuwa Mobutu wa Zaire au Bokassa wa Afrika ya Kati, atataka aendelee kutawala milele.

Rais Magufuli si mla bata. Jamaa dizaini hata pombe [no pun intended] hanywi. Sidhani kama anavaaga masuti ya bei mbaya.
Jamaa hata mamtoni huwa haendi.

Hata mkewe ukimwangalia unaona kabisa naye si mtu wa bata. Sijawahi kumwona kabeba sijui Birkin bags wala kuvaa red bottoms [Christian Louboutins]. Yeye ni mtu wa magauni ya vitenge tu na tu viatu twa kawaida.

Hata weave [wabongo mnaita weaving] yule mama sijawahi kumwona kashonea.

Hao si aina ya watu wapendao kukaa madarakani kwa muda mrefu.

2. Sidhani kabisa kama atataka kwenda down that rabbit hole.

Yaani yeye ndo aturudishe kule kwa zamani tulikotoka? Sioni kabisa hilo likitokea.

Jamaa atarudi zake Chato kwenda kuchunga ng’ombe.

Kwa hiyo, kwangu mimi hofu iliyopo ya kwamba atajiongezea muda, ni hofu isiyo na msingi wowote ule katika ukweli.

Najua kuwa huwa anapita humu maana kuna wakati aliwahi kunijibu kwenye moja ya hotuba zake baada ya mimi kuuliza humu kama alishawahi kufika Marekani 🤣.

Sasa, kwa jinsi alivyo, anaweza akapita humu na kuona nimesema kuwa hatojiongezea muda wa kubaki madarakani, na yeye akaamua kujiongezea ili tu afanye kinyume na nilivyodai mimi, ili nionekane nimekosea.

Don’t get it twisted, he can be petty like that.

Still, sidhani kabisa kuwa atajiongezea muda wa kubaki madarakani.

Na hii mada/ huu uzi, uwe ni kumbukumbu kuwa ‘NN alisemaga’.

Baadaye ✌🏿
 
Uchaguzi umeisha tutegeme 2025 tanzania kuwa kama ulaya au SA ccm watakamilisha miradi yote
Lami mpk vichochororoni,afya tatizo watalimaliza
Maji hakutakuwa na shida
Uwanja umebaki na wao wenyewe sasa

Ova
 
Kila kinawezekana Tanzania. Kama ingekuwa mzigo kama anavyodai asingekuwa anasema , "Si mtanipa jamani.

Kwanini wengine mliwapa 10 halafu mimi mnipe mitano tu jamani?" Sijawahi kuona mtu anabembeleza apewe mzigo mzito unless kuna maslahi mapana.
 
1. Kama Jiwe anaona uraisi ni Mzigo kwa nini amegombea the second term?

2. Kama unadhani hawezi kuturudisha tulipotoka kwa nini anaturudisha tulipotoka in so many ways, repressive laws, moves za kuua upinzani, kuminya uhuru wa habari etc
 
Kila kinawezekana tanzania. Kama ingekuwa mzigo kama anavyodai asingekuwa anasema , "Si mtanipa jamani. Kwanini wengine mliwapa 10 halafu mimi mnipe mitano tu jamani?" Sijawahi kuona mtu anabembeleza apewe mzigo mzito unless kuna maslahi mapana.
You are just nitpicking his speech!
 
Labda kwa sababu za kiafya, na umri mkubwa lakini sio kiatiba.

Hafuati sheria ila matakwa yake, akipendezwa ataongeza mpaka afie ikulu.
 
Kwa namna wale wabunge kule bungeni wanavyopenda kujipendekeza kwake, na vile anavyopenda kusifiwa, naona jibu sahihi litapatikana 2025 au hata kabla ya hapo.
Sahv miradi yote ya maendeleo itatekelezwa
Trust me 2025 tz itakuwa kama ulaya au dubai

Ova
 
Umenena vema mkuu. CCM kimekuwa ni chama chenye desturi nzuri ya kufuata Katiba, kanuni na miongozo yake.

Ifikapo 2025, CCM kupitia vikao vyake ya kamati kuu, halmashauri kuu na mkutano mkuu pasi na shaka atapatikana mrithi wa Magufuli.

Ifikapo 2025 Rais Magufuli atakua hana la ziada atakalokuwa kabakiza ikulu, miradi mingi mikubwa aliyoianza itakuwa imeisha au imetekelezeka kwa asilimia kubwa.

Atakuwa ameshasimama kwenye nafasi yake ya kuhakikisha Tanzania imejitambua kuwa inaweza kujisimamia kwa kila kiongozi kuwajibika.Ameshaonesha Mapinduzi ya kiutendaji kila mahali, atakachokibakiza ni kutuandalia mtu sahihi wa kuendeleza juhudi ambazo ataziacha.

Swali la kujiuliza ni nani atavaa viatu vya Magufuli. Lakini sina wasiwasi na yeye kuondoka kikatiba ifikapo 2025.
 
Back
Top Bottom