Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.Wizi mkubwa wa kura aliousimamia katika uchaguzi huu ni maandalizi ya project yake ya kubaki madarakani kwa kisingizio cha kusimamia white elephants zake, alishadokeza hilo
Let's go with facts.
1. Kulikuwa na wizi mkubwa wa kura. Lakini wizi huu ninkwa ajili ya muhula wa 2020 mpaka 2025.
2. Magufuli amesema mara kadhaa hataki kuongeza muda. Hakuna ushaidi kwamba ataongeza muda. Kumhukumu kwa kosa ambalo hajalitenda bado si sahihi. Magufuli ana makosa mengi sana aliyoyatenda, kaminya upinzani, kaiba kura, kaharibu biashara ya korosho. Mhukumuni kwa makosa ambayo kashayafanya, acheni kumhukumu kwa makosa ambayo mnafikiri atayafanya 2025 bila ushahidi. Mkianza kumhukumu kwa makosa ambayo mnafikiri atayafanya mwaka 2025, mnampa sababu na yeye kutumia kanuni hiyo hiyo ya kuhukumu watu kwa makosa ambayo hawajayafanya.
Atasema nimeota wapinzani watanipindua mwakani. Nawafunga jela wote.
Kumhukumu mtu kwa kosa ambalo hajalifanya kwa sababu unamshuku tu atalifanya ni jambo baya.