Je ulifanya kipimo gani kuhakiki ni vidonda vya tumbo?
Kipimo pekee kinachiweza kuthibitisha kikamilifu (confirmatory test) ni Upper GI Endoscopy, yani unawekewa camera kupitia mdomoni kuangalia njia ya chakula ikoje na kuona hivyo vidonda vipoje, vipo wapi na vimefikia hatua gani. Vyengine vyote si confirmatory tests. Je ulifanya hivi?
Wengi wanadhani wana vidonda vya tumbo kumbe magonjwa mengineyo kama Pancreatitis, Inflammatory bowel diseases, Esophagitis, Mallory Weiss Syndrome na mamia ya magonjwa mengine hata Cancer ya Mfuko wa chakula (Gastric Carcinoma).
Onana na daktari, fanya vipimo stahiki kisha tumia dawa kwa umakini, ukiona bado rudi kwa daktari wako.