Kwa aliyewahi kusikia kuhusu Bloody Mary

Kwa aliyewahi kusikia kuhusu Bloody Mary

Ngadu01

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2016
Posts
503
Reaction score
794
Dunia ina Maajabu.....

Habari, nimeileta mada hii jukwaa hili kwa sababu najua ndio sehemu husika.

Nakumbuka ni kama wiki tatu hivi zimepita nikiwa na rafiki zangu kwenye kiosk fulani hivi maeneo ya Ilala ndipo jamaa mmoja wa makamo mwenye asili kama ya asia alitukuta tunabishana kuhusu masuala ya mapenzi ndipo na yeye akaingilia kati akasema 'vijana msipate tabu mbona ni njia rahisi tu kumjua your future wife'

Mimi kwa shauku yangu nikaamuliza kivipi?ndipo akanipa maelekezo yafuatayo...
Aliniambia ikifika mida ya night kali nikiwa peke yangu chumbani niwe na apple jekundu nishike mkono wa kushoto pamoja na kitana mkono wa kulia simama mbele ya kioo tafuna apple huku ukichana nywele kisha sema''Bloody Mary×3 Please come i want to see my real wife..

Kiukweli nilipuuzia sikuchukulia sirious ila jana nikaona kwa nini nisijaribu kweli kidume nikanunua hizo zaga zaga ilipo usiku nikafanya kama nilivyoelekezwa dah aisee sikuamini nilichoona katika kioo changu mpaka nikaogopa baada ya kusema maneno hayo nikamuona binti fulani nilisoma nae ambaye mara mwisho kumuona ni kama miaka 7 sasa.

Nilipoamka leo asubuhi nikagoogle Bloody Mary ili kujua zaidi maelezo niliyakuta ni kwamba huo ni mzimu wa huko kwa wazungu na mpaka hayo yalitnikea yalichambuliwa pia.

Sasa ninachoogopa ni kwakuwa nimeuita huo mzimu hauwezi ukanitokea mara kwa mara?
anayejua zaidi atujuze nawasilisha tafadhali.
 
Nimewahi sikia hii lakini siamini sana
 
Subiri na mm leo nataka kujaribu alafu ntaleta mrejesho[emoji4] [emoji4] [emoji4]
 
Ni hatari Sana, Hizo kauli taarifa ni vizuri kufanyia uchaguzi kabla ya kufanya maamuzi
 
Jaribu mkuu uje elete mrejesho tuone kama yaliyomo yamo inaweza ikawa bahati xako ukamuona Kim Kardashian maana kuna tetesi Kanye anataka kupigwa chini haha
[emoji23] [emoji23] [emoji23] hunitakii mema ww kwanza hilo neno tuu BLOODY MARY[emoji124] [emoji124]
 
Ni cocktail . ..vodka na tomato juice na unaweza kuongeza Tabasco
bmary_cocktail.jpg
 
Katika pekuzi zangu pia mtandaoni leo nimekutana nayo hii wanasema ukinywa only three glasses unaweza kuwaona maghost live dah ni hatari sana
Ngadu01 umenichekesha kweli kweli na asante Kwa kuuita mzimu huo Tanzania . ....tutampa kazi ya kufanya . ..asante sana . .
 
Back
Top Bottom