SWALI: Mke/mme asiye mwema anatoka kwa nani? Nadhani sio kusali tu kunamfanya mtu apate mke/mme mwema; kama ilivyo sahihi kuwa taaluma ya mtu pekee haimfanyi awe mwanandoa mzuri. Historia ndiyo inadhibitisha kuwa taaluma fulani wako hivi, kabila fulani wako vile, n.k
Samahani mkuu, naomba nijibu hivi. Hakuna mke mbaya wala mume mbaya.
ILa kila mtu ana mke wake na kila mtu ana mume wake.
Wanadamu hatupo sawa,tupo tofauti, kiroho,kimwili, nafsi, kiakili, na kila kitu.
Ambacho tunakikosea tunawachagua wenza ambao sio wa kwetu, hamatch/halandani na wewe, hawezi kuchukuliana na matakwa yako,
haendani na wewe ulivyo. ILa mtu huyo huyo angekaa na mwingine wangeendana vizuri tu, wangeweza kuchukuliana, kumaliza tofauti zao, kujaliana na mambo kama hayo.
Kwa maana hio sasa, huwezi kumpata mtu unae endana nae kama hujamshirikisha Mungu kwa asilimia zote. Kwa sababu moyo wa mwanadamu ni mdanganyifu, siku zote. NItakubali kuolewa na ww coz nimechelewa kuolewa, naona una pesa na kazi so maisha yataendelea, unasali na unakwenda kanisani, nakuona mzuri wa rangi sura nk nk, unatoka kwene familia bora, ni bikra, hunywi pombe au sio mlevi.
Lakini nasahau haya, hivi huyu akikasirika naweza kuchukuliana na hio hali, hivi huyu akiwa na mastress naweza kuikabidhi hio hali au na mi nayaongezea mara mbili zaidi, hivi huyu mi nikikosea jambo ananisahihisha vipi, au yy akikosea anakubali je kosa na anachukua hatua gani nk nk nk nk nk
Maneno yanazidi kuwa mengi, lakini nahisi utakuwa umenipata walau kidogo.
Naishia hapo.