Brother Mimi nipo babati manyara Nina full vifaa yaani meza desktop complete ina 2terabyttes nawaza nianze kuifanyia kazi kinachonikwamisha ni wasiwasi wangu kuhusu usajili naomba unielimishe kidogo kuhusu kusajili hii biashara ya library ndogo ndio nataka nianze sijui nianzie wapi ili niisajili ni bei gani kuisajili na nikaenda kuisajili nawaambiaje? Kuhusu vitu kama tin no ninayo ya leseni ya udereva sijui kama inafaa naogopa kuanza bila kusajili naweza kamatwa na TRA maana naanza kufanyia kazi hii kibarazani tu naomba nieleweshe nielewe je naweza ifanya hii biashara pasipo kuisajili na nikafanikiwa au ni usajili kwanza ndipo nianze na ninapoenda kuisajili niwaambie kabisa mwamba nibiashara ya studio au niwafishe? Na bei ya kusajili ni shngap samahani naomba unichambulie hatua zote za kufuata hadi nifikie hatua ya kuanza ndugu yangu na pia nitakapokua tayari tu kuanza nitaanza kufanya kazi nawewe ndugu kuna ndugu wengi wako huko ntawaagiza wachukue mzigo wanitumie kaka pia nikushukuru maana mwanga umenipa wewe nilikua na machine ili nilikua naipuuzia nafanya nichek movie na miziki home tu bila kuifanyia kazi.. Naomba nisiandike essay sana niwasilishe kwako ndugu yangu..
mkuu kwanza nipende kukupongeza kwa kuamua kuingia katika utendaji kazi, lakini pili nipende kukushauri jambo unapokua ktk hii fani wakati unaanza wala haina shida unaweza ukafanya hata miaka na miaka bila kusumbuliwa na yeyote yule.
Binafsi nilikata vibali kwasababu tu ya mambo yetu bnadamu watu wakiona umefanikiwa basi ndio kila siku watabsha hodi kuja kufata mia mia zako unazotafuta.
lakini hapo kabla sikuwahi sumbuliwa na kibali wala mdudu wa TRA,japo wakati utafika kibali na TRA na leseni vitakua n lazima na wala sio ombi.
TRA wenyewe wana sehemu, na, sehem za kuingia hawaendi kila mahali,namna ulivyojiweka ndio utaita TRA au utawafanya wakuache, hivyo kwa sasa nashauri anza hivyo hivyo pga kazi walau miaka miwili hadi mi 3 bila kufanya chochote kile.
baada ya hapo ukishakolea wateja ukaswa na uhakika wakulaza 100k per day basi sasa wewe sio machinga tena n wakat wako wakukata leseni ya biashara na kujisajili rasmi.
unapotaka jisajili kwanza uwe na LESENI ya biashara (sio leseni ya gari) pili uwe na TIN NO (ya biashara) kisha utaenda BASATA ulizia chama cha LIBRARY/STUDIO/KUMBI ZA VIDEO utaelekezwa kisha ukifika huko wambie Biashara yako n library,watakupa kibali utacholipia kwa mwaka 20,000 na kuna vimalipo vingine (vya upgaji watakutajia) kuwa mpole we walipe ki ufupi hiyo siku itakatika hata 70k - 100k utamaliza usajili utawaachia paspot zako kisha utaambiwa lini ufate cheti chako,Kazi itakua imeishia hapo.
Hakuna jipya mkuu utakua umemalizana nao baada ya yoye hayo chukua namba zao za simu ikibidi hata ofisi nzima we beba namba zao za simu kila mmoja kwa wakati wake (utajua umuhimu wao siku 1) wakipga ziara zao za kushtukiza za hapa na pale kama huna connection wanaweza kukutia hasara (japo hii n nadra sana labda ungekua huku dar tena enzi zileeeee za bwana makonda na bongo movie wake)
ki ufupi mkuu hakuna jipya au la kushangaza kwasasa pga kazi kawaida hvyo hvyo kbarazani kwako usiogope mtu hakufati mtu na hatokufata mtu kweli zaidi ya yote STORAGE uliyonayo n kubwa inatoskha kuanza biashara na vfaa unavyo,ushndwe tu mwenyewe.
Karibu wakati wote utakapokua Tyari PM yangu ipo wazi kwa mawasiliano zaidi.