INAUZWA Kwa anayetaka kufungua biashara ya kuuzia watu filamu au nyimbo (softcopy) karibu tufanye biashara

Pamoja mkuu ....siwezi kumpangia jamaa miiko yake ya kufanya kazi nadhani hakunielewa ila mi serious nilikuwa nahitaji mzigo sema ndio ivo haikuwa ridhiki
 
Tuendelee kupambana vijana, nlichojifunza kutoka kwa huyu mwamba licha ya story mbili tatu tunazopiga
Asante sana sana sana Mkuu, nilitamani uje Utoe neno bila mimi kuku TAG maana nilihisi ningeku tag wasingechelewa kusema ni ID yangu nyingine.

Wote waliofanya kazi na mimi natamani siku waje kama ulivyokuja wewe watoe shuhuda zao, Asante sana Boss, nimefarijika kwa Feed back yako kweupe na hadharani.

Najua kadri siku zinavyoenda watakuja mmoja mmoja kutoa shuhuda zao,zaidi ya yote Boss umemaliza vyema sana hiyo paragraph ya mwisho ina ujumbe muhimu sana kwa kila atakae anza hii Biashara anatakiwa kuzingatia hili👇👇

Na mwsho zaid UVUMILIVU ni mtaj mwingne hasa kwa sisi tunaoanza. Usitangulize kuingiza elfu 50 wkt hujaandaa hayo mazingira.
 
Single Movies Zilizo Tafsiriwa

Kama ni kijana na hauna Storage ya kutosha lakini una Mashine (computer/laptop) Yenye HARD DISK only 500GB,

Una uwezo wa kufungua hii biashara ukajikita kwenye movie zilizotafsiriwa tu, uza movie 1 sh 300.

Utapata wateja wa kutosha na uhakika wakuondoka nyumbani na 10,000 kila siku ukiwa umeshakula na ushaweka vocha utakua nao kwa 81%.

Njoo nikuwekee movie za 500GB zilizotfsiriwa kwa bei nzuri sana nitakushauri na namna ya kupga pesa kwenye single movie hizi hizi.

500GB free space kama unayo usisite kuanza hii biashara,bado nawambia watu usiogope kuanza kwa kidogo ulicho nacho.
 
Single Movies Zilizo tafsiriwa zina wateja wengi zaidi kuliko ambazo hazijatafsiriwa.

500GB ya single zilizo tafsiriwa ni mzigo wa movie nyingi sana kwa kijana aliedhamiria kuifanya hii kazi.

Bei ya Movie unauza movie kwa ku VUNJA BEI wekea wateja single kwa 300Tsh tu,akija na buku muwekee movie 4.

Kwanini buku umuwekee 4,ili kesho tena aje na BUKU, wape kipaumbele wateja wanaokuja na buku buku zao.

Mteja akija na 500 akitaka movie, Muwekee movie 1 tu mpe chenchi yake 200, Fanya hivyo ili ajue kabisa ili apate movie ni lazima aje na BUKU.

pendelea wateja wanaokuja na BUKU kufika jioni utakua na uhakika kuliko mfanyakazi wa Kampuni Binafsi.
 
Mr HQ Natumaini ulifanikiwa kupata ushauri wa kukupa mwangaza wapi unataka kuelekea kuhusu ile biashra yako ya kukodisha Movie,nk
 
Kwa Wateja wa Majumbani, Nina Flash 32GB nauza kwa 20k

Flash inakua na Movie mpya (HD) imejaaaa

kuna Flash ya series na Movie,unaponunua Flash unaniambia nikuwekee nini kwenye Flash yako.

Vitu vya kuweka kweye Flash (series/movies) ni Free unachagua tu unataka movie zipi au series zipi Nakuwekea.

Bei ni 20,000 TU ukitoa 20,000 umemaliza,kazi inabaki kwako kuniandikia list ya most wanted series au movies unzozitaka kisha nikuwekee.

Wakazi wa DAR delivery Free mpka UBUNGO,Kwa wanaokaa mbali zaidi watalipia usafiri.
 
Kama Huitaji Movie unataka tu Flash mpya utumie mwenyewe

Reja Reja 32GB bei = 15,000
Jumla 32GB bei = 11,000 (kuanzia 5 kuendelea)
 
Hizi notes ni za bure kabisa. Sio rahisi hata mshikaji wako wa karibu kukupa nondo kama hizi kuhusu biashara yake, inayomfanya aishi.
 
Hizi notes ni za bure kabisa. Sio rahisi hata mshikaji wako wa karibu kukupa nondo kama hizi kuhusu biashara yake, inayomfanya aishi.
Nafanya hiviv ili kutoa mwanga kwa wanaotaka kuanza mkuu,hamna kitu mbaya kama kuanza biashara ukiwa hujui namna ya kuifanya.

Naepusha watu na hasara za kuweka "unwanted movies" kwenye store,kuna watu wana movie nyingi lakini ni "unwanted movies" na kuna watu wana movie chache lakini ni "wanted movies"
 
Maswali na majibu nakaribisha kwa wote wenye jambo ambalo linahtaji ufafanuzi
 
Maswali na majibu nakaribisha kwa wote wenye jambo ambalo linahtaji ufafanuzi
Brother Mimi nipo babati manyara Nina full vifaa yaani meza desktop complete ina 2terabyttes nawaza nianze kuifanyia kazi kinachonikwamisha ni wasiwasi wangu kuhusu usajili naomba unielimishe kidogo kuhusu kusajili hii biashara ya library ndogo ndio nataka nianze sijui nianzie wapi ili niisajili ni bei gani kuisajili na nikaenda kuisajili nawaambiaje? Kuhusu vitu kama tin no ninayo ya leseni ya udereva sijui kama inafaa naogopa kuanza bila kusajili naweza kamatwa na TRA maana naanza kufanyia kazi hii kibarazani tu naomba nieleweshe nielewe je naweza ifanya hii biashara pasipo kuisajili na nikafanikiwa au ni usajili kwanza ndipo nianze na ninapoenda kuisajili niwaambie kabisa mwamba nibiashara ya studio au niwafishe? Na bei ya kusajili ni shngap samahani naomba unichambulie hatua zote za kufuata hadi nifikie hatua ya kuanza ndugu yangu na pia nitakapokua tayari tu kuanza nitaanza kufanya kazi nawewe ndugu kuna ndugu wengi wako huko ntawaagiza wachukue mzigo wanitumie kaka pia nikushukuru maana mwanga umenipa wewe nilikua na machine ili nilikua naipuuzia nafanya nichek movie na miziki home tu bila kuifanyia kazi.. Naomba nisiandike essay sana niwasilishe kwako ndugu yangu..
 
mkuu kwanza nipende kukupongeza kwa kuamua kuingia katika utendaji kazi, lakini pili nipende kukushauri jambo unapokua ktk hii fani wakati unaanza wala haina shida unaweza ukafanya hata miaka na miaka bila kusumbuliwa na yeyote yule.

Binafsi nilikata vibali kwasababu tu ya mambo yetu bnadamu watu wakiona umefanikiwa basi ndio kila siku watabsha hodi kuja kufata mia mia zako unazotafuta.

lakini hapo kabla sikuwahi sumbuliwa na kibali wala mdudu wa TRA,japo wakati utafika kibali na TRA na leseni vitakua n lazima na wala sio ombi.

TRA wenyewe wana sehemu, na, sehem za kuingia hawaendi kila mahali,namna ulivyojiweka ndio utaita TRA au utawafanya wakuache, hivyo kwa sasa nashauri anza hivyo hivyo pga kazi walau miaka miwili hadi mi 3 bila kufanya chochote kile.

baada ya hapo ukishakolea wateja ukaswa na uhakika wakulaza 100k per day basi sasa wewe sio machinga tena n wakat wako wakukata leseni ya biashara na kujisajili rasmi.

unapotaka jisajili kwanza uwe na LESENI ya biashara (sio leseni ya gari) pili uwe na TIN NO (ya biashara) kisha utaenda BASATA ulizia chama cha LIBRARY/STUDIO/KUMBI ZA VIDEO utaelekezwa kisha ukifika huko wambie Biashara yako n library,watakupa kibali utacholipia kwa mwaka 20,000 na kuna vimalipo vingine (vya upgaji watakutajia) kuwa mpole we walipe ki ufupi hiyo siku itakatika hata 70k - 100k utamaliza usajili utawaachia paspot zako kisha utaambiwa lini ufate cheti chako,Kazi itakua imeishia hapo.

Hakuna jipya mkuu utakua umemalizana nao baada ya yoye hayo chukua namba zao za simu ikibidi hata ofisi nzima we beba namba zao za simu kila mmoja kwa wakati wake (utajua umuhimu wao siku 1) wakipga ziara zao za kushtukiza za hapa na pale kama huna connection wanaweza kukutia hasara (japo hii n nadra sana labda ungekua huku dar tena enzi zileeeee za bwana makonda na bongo movie wake)

ki ufupi mkuu hakuna jipya au la kushangaza kwasasa pga kazi kawaida hvyo hvyo kbarazani kwako usiogope mtu hakufati mtu na hatokufata mtu kweli zaidi ya yote STORAGE uliyonayo n kubwa inatoskha kuanza biashara na vfaa unavyo,ushndwe tu mwenyewe.

Karibu wakati wote utakapokua Tyari PM yangu ipo wazi kwa mawasiliano zaidi.
 
Kurudi nyumbani mida kama hii watu wa Movie Store ni kawaida,hatulali na hii ni mida ya kushusha kurasa za movie.
 
Asante sana kaka kwa maelezo yako nimeelewa vema sana kaka nitafanya hivyo kaka kama ulivyonielekeza ngoja nipambane pambane tutawasiliana kibiashara zaidi kaka nakushukuru sana bro

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…