INAUZWA Kwa anayetaka kufungua biashara ya kuuzia watu filamu au nyimbo (softcopy) karibu tufanye biashara


Mkuu iyo hela unanipa na external kabisa auu
 
offisi ya kawaida ila ukiambiwa gharama zake noma sana.
Watu hawa waheshimu waingiza miziki barabarani wanahisi ni vijana waliokosa kazi za kufanya kazi yao n kudownload nyimbo na kuingizia wateja (as if kudownload ni bure)

Heshima kwa jamii ya Tanzania kwa wafanyabiashara watu hawana kbsa,dharau na kejeli ndio zimewajaa watanzania walio wengi.
 
kweli kabisa
 
Halafu kuna watu humu wanakuja na ofa za Laki 4 mfano wa kina Nazi Ignition na wenzao wanaochukulia poa Movie store wanahisi ukiwa na Internet TU basi unaweza miliki Movie store na hutokosa movie yoyote wanafurahisha haswaa.

Root anakwambia ukiungwa na faiba ya 200k tu kazi kwishaaaa hahaha bwana Ruti ananipa amani sana nikisoma koment zake.

Hivi ukipata wateja wawili tu na Faiba yako ya 200k lazima utoke jasho hadi la ulimi?

Mteja wa kwanza anakwambia anataka Korean Drama inaitwa KING GWANGWAETO
Mteja wa pili anakuja anakwambia anataka Turkish Series inaitwa ERTUGUL

Ukiwapata wateja hao wawili tu na faiba yako ya 200k Jasho litakutoka mpaka masikioni,Mizigo yote hiyo ina download episode moja moja wateja washasubiri washachoka washasepa😅
 
hahahahahahaha umenifurahisha balaa.
umenikumbusha kuna sehemu nilienda kuchukua movie nikataja list 5 aise unaweza ona huruma.
 
Mkuu una uhakika hazipo au wewe ndio huna machimbo? Mimi sijihusishi na biashara hii ila ni mpenzi sana wa movies, series na music.. na hii biashara nitakuja kuifanya siku moja maana nina machimbo ya kila aina ya hizi movies, na kingine mkuu bei zako upo juu sana, ila niskupangie kaka ni maamuzi yako mkuu
 
Kwakua umesema utakuja anza hii biashara,nakusubir ukianza usisahau kurudia kusoma hii comment yako nimekuifadhia hapa.

Hamna site ya movie si ijui,na still kuna movie Sina na bando ninalo,kwanini sina? hili jibu utalipata ukianza fanya hii biashara.
 
hahahahahahaha umenifurahisha balaa.
umenikumbusha kuna sehemu nilienda kuchukua movie nikataja list 5 aise unaweza ona huruma.
Kuna list ngumu si rahisi rahisi,mimi kuna wateja nawambiaga wasije ofisini kama hawajanitumia list ya movie wanazotaka wiki 1 kabla.

yani kuna mteja anakutajia movie 20 na huna hata 1 as if ali igiza yeye na ndugu zake, yani anakutajia movie kwanza "mbayaaa" ila yeye ndio anazitaka na hata umwambie 2000 per movie analipia.
 
kuna mwingine nika mwambia aniweke kingsman 2, aise nafika home nakuta korea na ni chafu balaa, nilikasirika sana.
Huyu jamaa ana tabia mbaya sana,kanikumbusha mbaliii🤣
 
Kumbe Vunjabei ndo BOB PAAK
 
Sikuwahi jua
huwezi jua kirahisi na wanaojua ni sisi wenye movie store,Mimi nawajua wamiliki wa ofisi za movie store sio wafanyakazi zao.

na Ni wale wa Movie Store kubwa kubwa Tu ndio tunaojuana,Huwezi mkuta mmiliki wa Movie Store ofisini (ni nadra sana) ndio mana huwezi kujua nani mwenye nayo.

Na chat hapa JF ila huwezi nikuta hata siku 1 ofisni ni nadra sana kunikuta nimekaa ofisini,Mteja nitaempata ONLINE namuelekeza tu ofisini anaenda kukutana na vijana.
 
Maana yake Boss kawawekea kiwango cha pesa kila siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…