INAUZWA Kwa anayetaka kufungua biashara ya kuuzia watu filamu au nyimbo (softcopy) karibu tufanye biashara

INAUZWA Kwa anayetaka kufungua biashara ya kuuzia watu filamu au nyimbo (softcopy) karibu tufanye biashara

Wateja wa DAR

Flash 32GB = 17,000 (Ukinunua utajaziwa Movie au Series mpaka Flash ijae kwa bei hiyo hiyo)

External 320GB = 70,000 (Ukinunua utawekewa movie na series GB 100 free)

Flash FREE delivery "kuanzia Flash mbili"
External FREE delivery

Pesa utalipia kitu kikishakufikia ulipo,tunapeana kama ni kutest utatest kujiridhisha yaliomo yamoo au ni danganya toto.

Flash 16GB = 14,000

Kwa mahitaji ya STORAGE device zote tuwasiliane kwa bei ya JUMLA na REJAREJA.
 
We uko wapi njoo tushikiane tuifanye...
Kigoma town
kama mtaweza kushirikiana hii biashara n nzuri sana ni biashara ambayo NI LAZIMA sio ombi uwe na wafanyakazi au ofisi iwe na mtu zaidi ya m1,sasa mkiwa wawili na wote ofisi n yenu mtafanya kwa bidii na mtatengeneza pesa sana.

Japo pesa ikikolea Lazima mtagombana,Huo ndio ukweli. Kudumu milele haipogo hiyo ila kwa mwanzo sio mbaya mkianza pamoja ya mbeleni yatajijua yenyewe😂
 
@moviesstore

So mfano mimi nataka kuanzisha game center hapo hapo ni movie store, hapo leseni lazima ziwe mbili si ndio.

Na zote ni TRA
unakua na leseni na TIN ya biashara kAMA biashara zingine,kama na nyimbo unaingiza unakua na leseni na kibali pia toka TVLA.

Tanzania
Video
Library
Association

Hawa TVLA ndio wanao husika ktk kukamata kamata watu wanaoingiza nyimbo za wasanii bila vibali, wakikuotea hauna Kibali chao kukuchukua 500k ni jambo la kawaida sanaaa maana wanazungukaga na mapolisi na defender na wakija ofisini wanabeba mashine nzima na wewe wanakubeba.

Hawa ni kama (bwana pepsi) usiombwe kukutwa na hawa majamaaa wanatia hasara sanaaaaa, kama hujajipanga halafu ukakutana na hawa majamaa basi ndio mwisho wa hiyo biashara yako maana wako serious kuliko JAJI WA MAHAKAMA KUU.

Kama hutaki kero nao ili uwaepuke

-usiingize nyimbo za wasaniii wowote
-usiingize movie za Bongo
-kuwa serious na wewe,weka ofisi yako kiheshima (hawatokuja watapita kwa mbalii)

Ni hayo TU.
 
@moviesstore

So mfano mimi nataka kuanzisha game center hapo hapo ni movie store, hapo leseni lazima ziwe mbili si ndio.

Na zote ni TRA
Leseni ni 1 inayoonyesha unavyofanya ofisini kwako plus TIN ya biashara yako.
 
Biashara ya kurusha movie nimeifanya tangu mwaka 2011 mpaka 2014, baada ya hapo ikanipa connection ya kazi serikalini JPM alipo ingia madarakai msako wa vyeti feki ukaniondoa huko nikarudi kuifanya ndipo nikapata connectio kwenye kampuni ya wahindi , anay way ni story ndefu, naielewa changa moto zake, maswala ya kuliprishwa memory pale inapotafunwa na wadudu, mara computer kubooma, naona kwa sasa imenoka natamani kurudi tena kwenye biashara hii, ila miaka hiyo tulianza kwa ugumu kweli
Biashara tamu sana j3 naingiza 60000 kwanzia mda wa saa 11 jioni mpaka saa 5 usiku napo funga,yani naenda kulala macho yanawasha kinoma
 
Biashara tamu sana j3 naingiza 60000 kwanzia mda wa saa 11 jioni mpaka saa 5 usiku napo funga,yani naenda kulala macho yanawasha kinoma
Madha ra computee hayo,tafta miwani ya tinted ili kupunguza mionzi ya computer tofauti na hivo utakuwa kipofu asikwambie mtu, nilikuwa nikikaa na kitendo tu cha jua kuwaka machozi yananitoka, au baridi ikipuliza kidogo tu machozi hayo, nimesumbuka sana asikwambie mtu
 
Back
Top Bottom