Mkuu inawezekana una hoja ya msingi ila tambua unapozidi kujiweka imara wapo wengine wanatafuta mapungufu yako kwenye huo uimara. Cha ziada tambua kuwa hiyo ni biashara, unapoweka security kubwa watu wa software wanapata pesa zaidi nk.
Mfumo wa simu za android unatunza taarifa zote kwenye kifaa kama hdd ya kompyuta, ebu fikiria umeibiwa kompyuta mwizi akute umejitahidi umeweka security kwenye hdd si ataamua kuibadilisha na kuweka nyingine? Au akute komputa yako umeweke security ngumu kwenye bios si atatafuta saketi nyingine na maisha yaendelee?
Simu zilizonyingi za android zinatumia mifumo kama Lost mode, mdm, kg, anti theft nk ambapo simu ikiwa katika hali hiyo hauwezi kuiflash kwa mfumo wa kawaida, ila kuna mfumo wa programming kwa box za jtag na security zote zinatolewa na simu inatumika upya.
Kuna akaunti za kulock simu kama icloud, mi, oppo id na zinginezo ila bado watu wanazifungua na maisha yanaendelea.
Kuna wanaotumia signed IMEI files au OTP ila bado kuna solution ya kubadilisha. Ila kwa upande wa pili fikiria umenunua simu yako ya gharama kwa bahati mbaya security file zikafutika na ukapata null IMEI je, uitupe simu yako ukanunue nyingine kisa IMEI.
Kwa upande wa watengenezaji wanajitahidi kila wawezavyo ila kumbuka juhudi zao ndo ajira kwa wengine.