Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Ahsante kwa kunitaja.Wakuu na wataalaamu wa phone security,
Nini mtu afanye ili kuiwekea ulinzi smart phone ili itakapoibiwa ama kupotea aweze kuitrack?
Wezi wanaflash (factory reset) na kubadili IMEI number. IMEI NUMBER inapokuwa changed, habari kwishney, polisi wanakuwa hawana msaada wowote tena.
Je, kuna tracking app yenye uwezo wa kutoathirika na IMEI number change or hard reset? Mfano hizi simu za android family kama vile INFINIX, etc
Tupeane maujanja wakuu. Wizi wa simu unashamiri!! hasara inakuwa kubwa sana kwa wahanga.
IMEI International Mobile Equipment Identity) number ni namba pekee (unique) ya simu yako na kuibadili ni kosa la jinai.
Ndio maana katika nchi zilizo katika dunia ya kwanza, simu ikipotea na IMEI pia huandikwa kwa "blacklisted".
Hata hivyo IMEI namba ni rahisi kuipata ili kuweza kuwapatia polisi pale inapoibiwa kwa kupiga namba *#06# na IMEI kujionyesha bila shida.
Kwa sasa tracking app iliyopo ni ile ya "google trace my location" au ingine ya "find my device" ila hizi ni lazima simu yako iwe iko "on" wakati wote lakini yaweza kurekodiwa last location yake na mnara ulio karibu.
Njia ingine ya uhakika kabisa ni kuhakikisha wajiandikisha na Google account na kusajili simu yako/zako na taarifa zote muhimu zitawekwa pale zikiwemo IMEI number, model, manufacturer, kampuni unotumia na last activity ya simu yako.
Nafikiri ntakuwa nimekupa mwanga wapi pa kuanzia.