Kwa ardhi tuliyonayo tunashindwa nini kuzalisha alizeti tukawa wauzaji wa mafuta kwa Afrika

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Sehemu nyingi za Tanzania alizeti inastawi vizuri sana. Kuanzia Singida na hata maeneo ya Handeni. Wakulima wadogo wanalima na wanavuna.

Hawa think tanks wetu hawajaangalia uwezekano wa kufanya uwekezaji mkubwa wa zao hili kiasi cha kutoa ajira nyingi kwa vijana na pia kutiweka kuwa wauzaji wa kuu wa alizeti kwa soko la Afrika?

Ukraine waliwekeza sana kwenye zao hili na mziki wake tunauona baada ya hii vita kuanza. Pamoja na ardhi tuliyonayo, hata sisi ni wateja wa mafuta ya alizeti kutoka huko.
 
Hii nchi kipaumbele pekee ni mambo tusiyo na uhakika nayo,kuhusu kilimo bado sana

Akipatikana Rais Mmoja tu akafunga macho akakomaa na kilimo sio cha alizeti Tu ila kila zao

Tanzania tunatoboa,sio bandari sio nini itakuta income inayotokea kuptia kilimo n basi hajapatkana Rais mwenye Jicho la kuangalia wapi pesa ipo
 
Mitaji ndiyo inakwamisha wasomi kuji in giza katika kilimo cha kisasa kinachohitaji uwekezaji mkubwa.

Vijana wakijiunga kama 20 na waweke milioni tano kila mmoja, wapate ekari 300 na kulima alizeti wanaweza kabadilisha maisha yao na ya Watanzania wengine wanaowazunguka.
 
Alizeti pekee inatosha kututoa kimasomaso,hapo sijakwambia michikichi ya mafuta ya mawese,ukiacha mikoa ya Kigoma na Tabora michikichi pia inakubali maeneo mengi ya pwani.mawese yanatumika kutengeneza mafuta ya kula.
 
Shida siyo mitaji, ila bei kupangwa na serikali ndio inasababisha wakulima wengi kukimbia kilimo. Hebu imagine kwa sasa bei ya diesel ilivyo juu alaf nimelima tu alizeti kangu alaf mtu aje akupangie bei ya kuuza.
 
Mitaji ndiyo inakwamisha wasomi kuji in giza katika kilimo cha kisasa kinachohitaji uwekezaji mkubwa.

Vijana wakijiunga kama 20 na waweke milioni tano kila mmoja, wapate ekari 300 na kulima alizeti wanaweza kabadilisha maisha yao na ya Watanzania wengine wanaowazunguka.
Kwann serikali isituonyeshe Mfano maana ina rasilimali zote? Hii ingetupa chachu vijana kuweza kufanya hii kitu kwa kuangalia mifano hai tupate sehemu ya kujifunzia,Hamna kitu ngmu kama kufanya Practical wakati hujawahi hata kuona kwa macho practical ikifanyika zaidi ya kusoma tu theories.
 
Sehemu nyingi za Tanzania alizeti inastawi vizuri sana. Kuanzia Singida na hata maeneo ya Handeni. Wakulima wadogo wanalima na wanavuna.

Hawa think tanks wetu hawajaangalia uwezekano wa kufanya uwekezaji mkubwa wa zao hili kiasi cha kutoa ajira nyingi kwa vijana na pia kutiweka kuwa wauzaji wa kuu wa alizeti kwa soko la Afrika?

Ukraine waliwekeza sana kwenye zao hili na mziki wake tunauona baada ya hii vita kuanza. Pamoja na ardhi tuliyonayo, hata sisi ni wateja wa mafuta ya alizeti kutoka huko.
Watzn wako kama wewe hivyo yaani kupiga Domo tuu hakuna vitendo.

Who is Taifa?
 
Sehemu nyingi za Tanzania alizeti inastawi vizuri sana. Kuanzia Singida na hata maeneo ya Handeni. Wakulima wadogo wanalima na wanavuna.

Hawa think tanks wetu hawajaangalia uwezekano wa kufanya uwekezaji mkubwa wa zao hili kiasi cha kutoa ajira nyingi kwa vijana na pia kutiweka kuwa wauzaji wa kuu wa alizeti kwa soko la Afrika?

Ukraine waliwekeza sana kwenye zao hili na mziki wake tunauona baada ya hii vita kuanza. Pamoja na ardhi tuliyonayo, hata sisi ni wateja wa mafuta ya alizeti kutoka huko.
Kuna vitu viwili wafanyabiashara vs wawekezaji. Sisi tuna wafanyabiashara hatuna wazawa wa kuwekeza kwa muda mrefu. Tuna michikichi Kigoma ambayo tungeweza kutengeneza mafuta ya mawese ambayo ni mazuri kwa kutumia leo hii watu wanapata pressure,kisukari shida ni mafuta. Taifa linatumia gharama nyingi sana kwa sababu ya mafuta ya kula.

Na tatizo jingine kubwa ni viwanda vya ndani mafuta nayo ni bei ghali sana bora ukanunue mafuta ya nje. Tunayo safari ndefu mifumo yetu ipo wazi.
 
Mitaji ndiyo inakwamisha wasomi kuji in giza katika kilimo cha kisasa kinachohitaji uwekezaji mkubwa.

Vijana wakijiunga kama 20 na waweke milioni tano kila mmoja, wapate ekari 300 na kulima alizeti wanaweza kabadilisha maisha yao na ya Watanzania wengine wanaowazunguka.
Serikali inatoa pesa za mitaji ila watu wanataka kubet tuu mjini.
 
Mkuu hii serikali haioni kama kilimo ni shughuli ya muhimu kwa watu,yani pembejeo saizi ni bei Sana lakini bado ukifika muda wa mavuno mkulima anapangiwa bei,tangu nilipopata akili nilishaidhinisha kuwa kilimo kifanywe na wenye pesa wapeleke mazao nje wakauze ila kwa asie na mtaji wa maana atapoteza muda.
 
Hii nchi kipaumbele pekee ni mambo tusiyo na uhakika nayo,kuhusu kilimo bado sana

Akipatikana Rais Mmoja tu akafunga macho akakomaa na kilimo sio cha alizeti Tu ila kila zao

Tanzania tunatoboa,sio bandari sio nini itakuta income inayotokea kuptia kilimo n basi hajapatkana Rais mwenye Jicho la kuangalia wapi pesa ipo
Kwanza tukiwekeza kwenye kilimo tunaweza kwama kwingine lakn kwenye swala la msingi na la kwanza kwa mwanadamu tutakuwa tumelitatua 100% ambalo ni chakula kwanza.

ila bongo zetu zimelala sana.

Mzee Rungwe walikuwa wanamuona kichaa lkn kwa jicho lingine alikuwa na hoja.😄
 
Kwann serikali isituonyeshe Mfano maana ina rasilimali zote? Hii ingetupa chachu vijana kuweza kufanya hii kitu kwa kuangalia mifano hai tupate sehemu ya kujifunzia,Hamna kitu ngmu kama kufanya Practical wakati hujawahi hata kuona kwa macho practical ikifanyika zaidi ya kusoma tu theories.
Uwekezaji mkubwa wa sekta binafsi Ethiopia unafanywa na wazawa hasa wali o Ughaibuni, wengi walipata ukimbizi miaka ya 80-90 na sasa wanaamua kuwekeza nyumbani kwao. Wengine wamefungua viwanda vya viatu na Mikoba ya ngozi kutokana na upatikanaji wa ngozi kuwa mkubwa nchini mwao.
 
Sehemu nyingi za Tanzania alizeti inastawi vizuri sana. Kuanzia Singida na hata maeneo ya Handeni. Wakulima wadogo wanalima na wanavuna.

Hawa think tanks wetu hawajaangalia uwezekano wa kufanya uwekezaji mkubwa wa zao hili kiasi cha kutoa ajira nyingi kwa vijana na pia kutiweka kuwa wauzaji wa kuu wa alizeti kwa soko la Afrika?

Ukraine waliwekeza sana kwenye zao hili na mziki wake tunauona baada ya hii vita kuanza. Pamoja na ardhi tuliyonayo, hata sisi ni wateja wa mafuta ya alizeti kutoka huko.
Chini ya akili finyu za CCM hamna kitakachofanikiwa.
CCM wanaamini eti mwenge unaleta amani ukikimbizwa, waupeleke sasa Ukraine 🇺🇦 ukalete amani
 
Tukipata Watu watano, wakawa tayari kutoa 5m Kila Mtu na tukajiunga na ku-process loan bank tunaweza kukusanya 50m Hadi 100m, hii tunaweza kuweka kwenye Alizeti tukafanya wonders. Tukipata 1b tunafanya kilimo Cha umwagiliaji bila kumtegemea Mvua, meaning kuwa Kunakua na stable and quaranteed supply ya Alizeti.

Nimefika Kondoa, Kuna kiwanda Cha Mafuta ya Alizeti, ameshapumzika kwa Amani yule Mzee ila ni uwekezaji mkubwa japo hakifanyi kazi Tena Kwa sasa.

Water table Iko juu sana ukanda wote wa Dodoma, Singida hata baadhi ya maeneo ya Tabora na Shinyanga kwahio irrigation system ni Rahisi sana na pump unafunga za solar.

Sunflower husks ni raw materials ghali sana sana na most of the time zinakua exported. Kwahio huuzi Mafuta tu unauza Hadi hayo mashudu kwa Ajili ya break pads na chakula Cha mifugo....nani Yuko Tayari?
 
Back
Top Bottom