Kwa ardhi tuliyonayo tunashindwa nini kuzalisha alizeti tukawa wauzaji wa mafuta kwa Afrika

Kitu cha muhimu ni mnunuzi atakae kuwa tayari kusafirisha au kusindika hapa hapana kuuza mafuta.
 
Alizeti pekee inatosha kututoa kimasomaso,hapo sijakwambia michikichi ya mafuta ya mawese,ukiacha mikoa ya Kigoma na Tabora michikichi pia inakubali maeneo mengi ya pwani.mawese yanatumika kutengeneza mafuta ya kula.
Mawese tatizo lake harufu tu aisee
 
NCHI hii sio maskini, ina kila kitu. Tatizo, haya tunayoyaona ni matatizo ya kutengeneza ili wengine wale. Watu wana create crisses fulani ili waendelee kupiga pesa that's one. Secondly, viongozi wengi tulionao hawana uwezo wa kutatua changamoto hivyo huwa rulers badala ya kuwa leaders.
 
Nina Imani kama bajeti ijayo wataitekeleza kilimo kitapiga hatua ila isiwe ni mwaka wa fedha ujao tu iwe endelevu. Lakini pia wadau tusiwalaumu wasomi kujiingiza kwenye kilimo kwa ukosefu wa mitaji tutakuwa tunakosea sana. Kilimo kama biashara nyingine inahitaji mtaji, maarifa na muda.
 
Tatizo ni kwamba nchi yetu haina sera ya kuaminika kuhusu kilimo, kila anayekuja anakuja na project ya agriculture, mara kilimo kwanza, mara mapinduzi ya kilimo, mara hivi mara vile. Hakuna sera za kuaminika. Viongozi huingia madarakani na kuanzisha projects za kilimo ambazo hudumu kwa muda fulani kisha hupotea na lengo kubwa huwa ni kwaajili ya upigaji tu kuchukua mapesa huko World Bank mara IMF kwaajili ya hizo project, wakifanikisha kupiga pesa ndio imetoka hiyo. Sisi Tanzania and Africa at large hatupo consistent kwenye jambo moja kung'ang'ana nalo hadi lifanikiwe issue ni kukosa sera za kuaminika. Mara tupo kwenye kilimo, mara chuma, mara gas, mara korosho yaani tunarukaruka tu mithili ya maharage yasiyotaka kuiva sufuriani.
 
Soko la alizeti liko wapi .. mkuu
 
Hata elimu yetu inatuacha nyuma katika soko la kimataifa la ajira.
 
Sera mbovu,sie tunajua kununua wanasiasa na propaganda za chama tawala tu,Malaysia walichukua mbegu za mawese kutoka Kigoma,leo wanauza mafuta ya kula Dunia nzima,Kuna mbwembwe sana nchi hii,mala utasikia kilimo kwanza,nchi ya viwanda,gari za nyumbu,lakini tunashindwa kuwekeza kwenye kilimo Cha alizeti,juzi tumewapa wachina ekari 2500 za kilimo,kwanini sie hatuibadilishi Singida iwe sehemu ya kuzalisha mafuta kwa nchi nzima,
 
Uzalishaji mkubwa utazalisha ajira na kuongeza walipa kodi, hata kama ni kwa mkopo ni muda tu mkopo utalipika.
 
kwasababu tatizo si ardhi, tatizo ni kilimo na biashara... ni km vile tulivyo na vivutio vingi na vizuri vya utalii kuliko kenya but kenya wanaenda watalii wengi kuliko tz, Issue sio kuwa na vivutio tu ni namna tulivyojipanga kwe biashara, kwa mtazamo wngu hp ndio penye changamoto
 
Unaongelea alizeti wakati ngano tu eti Tanzania inaagiza kutoka nje!! Bei ya unga imepanda maradufu wakati maeneo ya kulima tunayo... Point kubwa kwenye suala la alizeti Ni research chache na Tija ndogo kwa wakulima. Ukilima eka Moja ya alizeti na mahindi, faida ya mahindi Ni kubwa kuliko ndo Mana tuna changamoto. Serekali inahitaji kutafiti shida nini, Ni Bei ndogo ya alizeti kwa wakulima au mbegu tunazotumia Ni duni? Ila serekali isome kwa Ukraine kwa Nini wait wanafanikiwa...
 
Swali lipo hapa, Bei ya alizeti Ni ndogo kweli! Sababu Ni ndo Bei ya soko la dunia au tija kwenye ekari Ni ndogo kiasi kwamba mtu akiuza kwa Bei hiyo elekezi hapati faida ya kutosha?
Shida siyo mitaji, ila bei kupangwa na serikali ndio inasababisha wakulima wengi kukimbia kilimo. Hebu imagine kwa sasa bei ya diesel ilivyo juu alaf nimelima tu alizeti kangu alaf mtu aje akupangie bei ya kuuza.
 
Wasomi hawajawahi kua na shida na Mitaji, shida zao"
1.kutokua Risk takers( tuna calculate risk sana)
2. Uoga wa kufeli( whatif)
3. Kilimo cha whatsapp(pigwa sana na wasimamizi wa mashamba)
4. Kukifanya kilimo km side income, hivyo ku pay attention kubwa na kazi ya kuajiriwa kuliko kilimo.
5. Kuanzia kilimo shambani instead ya sokoni kujua soko likoje kabla ya kuanza kilimo(disapointement during selling)
6. Kukata tamaa mapema(hii inachangiwa na kua na uhakika wa salary)
 
Hiyo milioni tano tano waitoe wapi wakati tayari wamechakazwa kwa viboko vya CCM?
 
yaeh, research ni muhimu sana, kuanza kwe kilmo chenyewmpk biashara yake
 
Ccm na tiss yao kikubwa walichonacho kimataifa ni kumuwinda Tundu lisu nakukwapua mabegi yake Basi.....mengine Kama uliloona wewe haka hawana habari nalo
CCM ina watu wa hovyo sana, ndio chanzo cha kuzalishwa kwa MAMILIONI YA MAKAPUKU hapa nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…