Kwa asilimia nyingi Waislamu tumechukua tamaduni za Kiarabu. Je, Uislamu ni Uarabu?

Kwa asilimia nyingi Waislamu tumechukua tamaduni za Kiarabu. Je, Uislamu ni Uarabu?

u

taratibu za Kuoa - Kuvaa kanzu huku kiunoni kuna jambia la vitani kudhani ndio uislam. ?

Kwanza kumbuka, katika Uislam hakuna "kuoa" kuna kuoana.

Hakuna wepesi wa kuoana kama katika Uislam.
Kuoana Kiislam ni mume, mke, walii, na mashahidi wawili. Mengine ni tafrija tu za harusi, hazina uhusiano na kuoana.

Kila mmoja anafanya tafrija yake apendavyo.

Hata Mmasai haendi kuoa bila sime na rungu na fimbo.
Hiyo ni 'symbol" ya kuonesha kuwa hata huku unakokuja utapata ulinzi. Isikupe shida.
 
Kutukuza waarabu - kuwa na dhana potofu kwamba waarabu ni ndugu zake Mwenyezi Mungu, kuiita ngozi ya kiarabu ngozi ya mtume, mwarabu akitaka kitu flani ni ngumu kumkatalia, akikosea kitu flani rahisi kumsamehe.
Hayo yote unayasema wewe kwa kujidangaya. Muisla anamtukuza mmoja tu, ndiyo maana unaisikia ile "Allahu Akbar".

Mengine yote hayo uliyoandika hayana mashiko, Uislam pekee ndiyo unafundisha mbora kati yetu ni mcha Mungu, siyo kabila lake wala mali yake wala chochote kile chake.

Uislam ni mwema sana.
 
lugha - Kusoma quran kwa kiarabu hata kama huelewi, kusalimiana kwa kiarabu, n.k.
Ma shaa Allah, kitabu cha Qur'an kilishushwa kwa lugha ya Kiarabu, mpaka leo kipo hivyo hivyo orijino, dunia nzima utapokuta Waislam watasali na kukisoma namna moja. Huo ni muujiza unaoishi na wewe.

Hiyo inalindwa na Mwenye Allah, ingekuwa kwa mapenzi yako, isingekuwepo leo, taama vido clip hiyo chini, utaelewa kuwa huo ni muujiza unaolindwa na Allah.

Soma Qur'an kijana ufaidike, kama hujuwi Kiarabu, anza japo tfsiri yake Kiswahili, ujionee aha yake.

Hii hapa: Qur'ani Tukufu


 
Back
Top Bottom