YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 52,001
ndio exactly lakini wakiwa na lao mfano sijui ujenzi wa kanisa au michango huzunguka kuomba hadi kwa wapagani wachangie!!Wabinafsi.....??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ndio exactly lakini wakiwa na lao mfano sijui ujenzi wa kanisa au michango huzunguka kuomba hadi kwa wapagani wachangie!!Wabinafsi.....??
Kama mtu binafsi pamoja na ndugu plus marafiki wana hali nzuri ya uchumi sioni ubaya wowote wa kutumia millions. Jikune pale mkono unapofika.Kwanini utumie mamillion kwa shughuri ya siku moja![]()
Anayekimbia hajakupendaNi Jambo jema lakini kwa Karne hii mtihani mkubwa ni kumpata mwanamke atakayekubali kufunga ndoa bila sherehe kubwa. Wengi wanataka sherehe ya kifahari, msafara wa magari na miosho mingi ili mji mzima wajue kuwa ameolewa. Ukigusia swala la ndoa bila sherehe wanakukimbia
Tunachokereka nii kutusumbua michangoKama mtu binafsi pamoja na ndugu plus marafiki wana hali nzuri ya uchumi sioni ubaya wowote wa kutumia millions. Jikune pale mkono unapofika.
Kama hauna pesa mwambie mtu ukweli kwamba, "ndugu yangu hongera kwa kuamua kufunga ndoa lakini mimi nipo katika hali mbaya sana ki-uchumi"Tunachokereka nii kutusumbua michango
...kubaliana na mwenzako, itisheni wazazi na mchungaji, tawanyikeni
Tena na upendo wa Mungu kati yaona Mungu akawajaze rehema daima.
Ndoa hizi zimeshuhudiwa na maelfu ya watu; na kati yao ni ndugu na marafiki zaoMi nadhani ndoa inahitaji kushuhudiwa na watu kama ishara ya baraka pia. Kama bible imeweza kuhusianisha tukio la kuokolewa na bwana kama ni mfano wa harusi na kila jicho litashuhudia nadhani its a blessing zaidi watu wakishuhudia.
Ilikuwa siku ya Ijumaa 19.2.2021, ni siku nyingine ya kukumbukwa, katika Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Dar-Es-Salaam, lililoko Barabara ya Sam Nujoma; pale ambapo jumla ya wahusika 84 waliposhiriki katika kufungwa kwa Ndoa 21, zilizofungwa kwa pamoja katika Ibada ya Ndoa iliyoanza saa 5 asubuhi. Wahusika hao 84, walikuwa ni Mabwana Arusi 21, na Mabibi Arusi 21, ambao hawajawahi kuishi pamoja; na jumla ya Mashahidi 42 (waume 21 na wake zao 21).
Kama ilivyo ada, katika Arusi hizo, viwango vya mavazi ya Mabwana na Mabibi Arusi, vilikuwa ni vilevile ambavyo vimekuwa vikizingatiwa, katika Ndoa mamia kwa mamia, zilizofungwa katika Kanisa la FGBF, kwa miaka zaidi ya 30; hususan tangu Askofu Mkuu Zachary Kakobe alipoliasisi Kanisa hili, tarehe 30.4.1989.
Katika Ibada hiyo ya Ndoa, Askofu Kakobe alihubiri kwanza ujumbe wa Neno la Mungu lisiloghoshiwa, wenye kichwa, "WALA MSIIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII" (WARUMI 12:2); kisha ndipo alipofungisha Ndoa hizo 21 kwa pamoja.
Suala lililowavutia sana wageni, waliohudhuria kwa mara ya kwanza, katika Ibada za Ndoa za Kanisa la FGBF, ni jinsi walivyowashuhudia Maarusi hao, wakitumia usafiri uleule wa kawaida ambao wamekuwa wakiutumia, wanapokwenda Kanisani, katika Ibada nyingine za kawaida. Baada ya kufunga Ndoa zao, Bwana Arusi mmoja mwenye gari lake, alikwenda na mkewe, nyumbani kwake, na gari lake hilohilo, huku akiliendesha mwenyewe.
Baadhi ya Maarusi, walikwenda kwao, kwa kutembea tu kwa miguu, huku wameshikana mikono kwa upendo na furaha isiyoelezeka; na kuwasisimua watu wengi. Siyo hilo tu, Maarusi wengine wengi walitembea kwa miguu, huku wamejaa bashasha, mpaka kwenye kituo cha daladala kilichoko jirani na Kanisa hilo, na kupanda daladala hizo zilizowapeleka majumbani kwao. Taarifa zilizopatikana baadaye, zinaeleza jinsi baadhi yao walivyokuwa wakihubiri Injili ndani ya daladala hizo walizozipanda.
Bwana Arusi mmoja, ambaye hutumia pikipiki (bodaboda) yake kuja Kanisani, alimvisha helmet (kofia ngumu) mkewe, kisha akampakia mkewe (Bibi Arusi), kwenye bodaboda hiyo, na kuondoka naye kwenda nyumbani, huku watu wengi walioshuhudia tukio hilo, wakishangilia kwa nderemo, vifijo na vigelegele !
"Basi atukuzwe Yeye (Mungu) awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina" (WAEFESO 3:20-21). MARANATHA !!!
Tazama picha zao
View attachment 1708770
View attachment 1708771View attachment 1708772View attachment 1708773View attachment 1708774View attachment 1708775View attachment 1708776View attachment 1708777View attachment 1708778View attachment 1708779View attachment 1708780View attachment 1708781View attachment 1708782View attachment 1708783View attachment 1708785View attachment 1708786View attachment 1708787View attachment 1708788View attachment 1708789View attachment 1708791View attachment 1708792View attachment 1708793View attachment 1708794View attachment 1708795View attachment 1708796View attachment 1708797View attachment 1708798View attachment 1708800View attachment 1708801View attachment 1708802

Mimi siko huko kwenye pombe, mimi nasema Yesu alkuwepo kwenye harusi yaani ukumbini kwenye sherehe, na alitoa mchango wake kwenye hiyo harusi kwaiyo harusi ni kitu cha baraka.Si kila neno katika divai katika Biblia maana yake ni pombe kama wengi wanavyofikiri lazima pombe iwepo katika sherehe zao kama hizi std7