sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Yes, eminem kuna muda anasifia kwamba kuna marapa weusi flani walikuwa anawasikiliza, wanampa morali, n.k lakini hii haiondoi ukweli kwamba yeye ni mfalme, Messi anaweza kumsifia Maradona alikuwa bora lakini haiondoi ugalisia kwamba Messi ndie mfalme,
Laiti Eminem angekuwa mweusi angekubalika kirahisi sana na kuwa Muhamed Ali wa Hiphop.
Marapa weusi tayari wana platform kwa watu weusi kuwa na utayari wa kusikiliza ngoma zao , hata kama ngoma ni ya msanii underground basi ana ka platform tayari ka wasikilizaji weusi,,, kwa eminem maana hali ilikuwa tofauti hakuwa na hii platform, watu weusi walikuwa hawana shauku ya kusikiliza ngoma zake, ilimbidi Eminem atie kishindo ndio watu wageuke kumsikiliza, alianza na freestyle hizi miaka ya 90's alkuwaa anawachana bila huruma watu waliodiriki kuomba battle, haikuwa rahisi aisee , marapa weusi ni kama wachezaji wa Yanga / Simba tayari wana platform za mashabiki hata kama wana uwezo wa kawaida, Eminem ni kama George mpole msimu uliopita hakuwa na platform ila aliwika kwa kufunga magoli mengi.
kina 2pac na bigi walikuwa vizuri lakini naweza kusema vifo vyao viliwakuza zaidi majina yao, pac na biggie majina yao yalikuzwa maradufu kwa mabifu na vifo vyao, halafu bora 2pac hata alikuwa na nyimbo za kuelmisha jamii na kuleta mabadiliko chanya, bigi kwa pac hafui dafu labda vitu vichache.
Hakuna rapa anaetaka bifu na Eminem, Ukijaribu anakutungua juu juu ukifika chinii chali, Wasanii wakuwa tu kama kina The game, 50 cent walishaweka wazi hatua za kuchukua ukiwa na bifu na Eminem ni kumkwepa tu yaishe. Eminem hakuchani kwa mistari pekee, anakuharibia career moja kwa moja,,, wapo wapi kina Jarule, kina machine gun kelly, n.k.
Anaweza kuyachezea maneno kwa style za kutuacha mdomo wazi, freestyle anazicharaza, rap battles wapinzani wanakimbizwa, ni dubwana linaloikunja mistari kadri atakavyo, speed a kurap kasgaunja rekodi huko, freestyle ndo usipime