Kwa bajeti ya milion 2 niwekeje ghetto liwe Kali?

The dumb Professor

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2023
Posts
852
Reaction score
1,978
Wataalam,

Asiwadanganyeni mbwa yeyote kukaa kwa baba mkwe jau sana...Hii nyumba nayoishi masaki ni ya baba mkwe, Sasa juzi kati luku iliisha nikampigia kumuomba anunulie nyumba yake umeme,looh hayo maneno niliyomwagiwa ni heri kumwagiwa maji ya ukoko.

Sasa kwa hasira nachofanya mshahara ukitoka tu, nina mpango wa kuhama hapa nitafute ghetto la kukaa kisingle boy. Na binti yake ntamuacha.

Sijawahi kupanga hapa Tanzania na Sina experience yoyote ya vyumba huku vikoje. Maana nilipomaliza high school nkaenda kusoma nje na nimerudi juzi tu nikaanza kukaa kwa baba mkwe.
Hiyo 2M ni ya mshahara utakaotoka mwezi huu.

Sasa wakuu naombeni mnipe mbinu niipangiliaje hiyo hela nipate Kodi ya ghetto(maeneo karibu na posta/daladala moja) pia na vitu vya kuanzia ndani.
ili hata nikiingiza mrembo akipaona anase/agandie.
(Maana huyu Binti niliye naye Nina mpango wa kumbwaga nikihama kwao.)

NB:Kitanda na godoro ninavyo. Hapo hio hela ni ya Kodi na mazagazaga mengine ya kupendezesha ghetto.
 
Ntakua nikiwa ndani ya ghetto langu, we kwa Sasa nielekeze niipangiliaje 2m ghetto lipendeze akiingia mdada ang'ang'anie
Tafuta mikocheni huwezikosa single self room ya 200k per month lipa mwaka unabakiwa na laki 8 then kwa kua umesema G& Kitanda unavyo nunua Fanicha za walau laki 5 ambayo ni maybe set ya viti kadhaa na kimeza cha normal then baki na laki 2 ya nauli za hapa na pale ili ukimwaga bisi za mjasiriamali pale mataa ya Morocco uweze kujitetea Ova!

NB: Hapo mikocheni utakapopata ni dala 1 popote waenda plus ulinzi upo wa kutosha no uswahili

Mungu akutangulie
 
Hio single ya laki2 inakuwa self? inakuwa na space ya kuweka Hzo meza,vitu godoro Kitanda na baadae friji,na mambo mengine? Yan inakuwa na ukubwa gani?
 
Kuna watu mnaroho ngumu sana Aise,, UNAKAA KWA BABA MKWE 😳😳😳.
 
Kuna watu mnaroho ngumu sana Aise,, UNAKAA KWA BABA MKWE 😳😳😳.
Yani iko hivi, nilikuwa nasoma USA nikakutana na Dem mbongo tukapendana, kumbe ni mtoto wa kigogo ...tuliporudi bongo akasema ana nyumba kubwa tu masaki hawezi kukaa mwenyew akaomba tuishi wote, nkawa nakaa nae kwake. Kumbe hiyo nyumba alipewa na baba ake.
Nilikuwa kujua baadae kumbe hati unasoma jina la baba ake

Sasaivi Binti aliondoka akaenda Ulaya kwa ishu zake binafsi,kaniacha apa naishi kwenye hii nyumba niliyojua yake kumbe ya baba mkwe
 
Chukua hiyo Million mbili, nunua LUKU ya laki 5, weka. Endelea kuishi.
Amna mzee....saivi nataka kwanza niachane na huyu Dem....
Nataka nitafute ghetto niwe nabadilisha pisi Kali tu maana hapa nimebanwa sana.
 
Duh, pole sana AISE, kitu kinacho itwa mwanamke, usiwaamini sana mkuu..
 
Take home milioni mbili nyumba ya bure masaki unashindwa kulipia Luku unayotumia mwenyewe ba mkwe kaona hii hassara
Na wenye akili wameona hii ni chai
 
Sasa mkuu una mahahara 2m unaombaje luku lakini
 
Million mbili haitoshi fanya chochote utaishia nunua pazia na godoro tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…