Kwa Bajeti ya Mwaka Mmoja tunaweza kuziunganisha Tanganyika na Unguja kwa barabara

Kwa Bajeti ya Mwaka Mmoja tunaweza kuziunganisha Tanganyika na Unguja kwa barabara

SankaraBoukaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2019
Posts
1,213
Reaction score
1,918
Iko hivi, umbali mfupi kati ya Tanganyika na Unguja ni karibia Kilomita 40 ambazo ni sawa na kutoka pale Makutano ya Mataa ya Magomeni Hospitali mpaka Kibaha kwa Mathias.

Uchimbaji na Ukwanguaji wa kisasa wa miamba chini ya bahari kwa kutumia TUNNEL BORING MACHINE inayoweza kukwangua karibia Kilomita 30 kwa siku itachukua miaka kama mitatu (3) endapo hakutakuwa na changamoto.

Gharama za Ujenzi wa hili Handaki unakaribia bajeti ya Tanzania kwa mwaka mzima yaani Trillioni kama 38 hivi...

Kupanga ni Kuchagua,,, kipindi cha awamu ya 3 kuna Kiongozo aliwahi tuambia tule nyasi ili tununue Ndege ya Rais sasa mnaonaje tuwe wazalendo tukajipunja nusu bajeti kwa miaka miwili mfulululizo tujenge hili HANDAKI?

#ANGALIZO:
Sina Elimu ya Uhandisi wala Uchumi, mimi ni kama Darasa la Saba (7) nayeruhusiwa kubishana na Maprofesa Bungeni.
 
Sasa mkubwa katika huo mwaka inabidi kila kitu kisimame kupisha ujenzi wa barabara ya kwenda zanzibar, hii ni pamoja na hakuna kununua madawa hospitalini hata panado, hakuna kulipa mishahara watumishi wote narudia tena wote kuanzia waalimu, mapolisi na kina Denis Urio. Hakuna kujenga hata sentimita moja ya barabara nchi nzima na mwisho ma V8 ya viongozi yote yasitemnbee kwa mwaka mzima, sorry nilisahau na hakuna bunge kukaa maana hakuna posho

Ila wazo zuri mkuu, tupigie debe mwana tuwe tunaruka zenji na ist zetu chap! unanunua viungo vya pilau unageuka home Tabata
 
We unadhani inashindikana hiyo project hata kwa kukopa ila kuna watu wana maslahi yao hawawezi kukubali swala hlo kwanza boat tu hataki kampuni nyingine zaidi ya yakwake atakubali kweli hlo yule mzee anayejifanya swala tano.
 
Mafisadi wakiacha wizi haizidi miaka 5 tutakua tumeshakusanya pesa za kujenga hiyo barabara
 
Iyo hela inaweza jenga 29,230km za lami uku tz bara. Hapo 1km ijengwe kwa 1.3b tzs

Sasa zanzibar kunafikika kwa meli boti na ndege kwann tu-waste fedha nyingi kiasi hicho?
 
kwa sasa.. boti inatosha mana ni fasta tu pia mtu unafik unguja japo gharama z usafiri n kubwa kulnganisha kama kungekuw n daraja.
 
Back
Top Bottom