Kwa binti mwenye umri mkubwa acha hizi tabia unapompata mwanaume mwenye nia ya kukuoa

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Naongea na mabinti wa miaka 35 au zaidi. Huu umri kama upo single ni mkubwa kwa mwanadada hivyo kuna mambo lazima ukubaliane nayo kuwa hayapo upande wako kwa sasa. Ukishupaza shingo shauri yako.

Endapo umepata mwanaume aliye tayari kukuoa mwenye umri kukuzidi lazima ukubali kuwa hakutakuwa na mambo kama ya wapenzi wenye umri mdogo (under 30s).

Mtu mwenye umri huo hawezi kuwa na mambo ya kukutumia message za umekula? Umevaa nini? Au zingine za kitoto. Vinginevyo utafute Mario mwenye umri mdogo ili akupe attention za namna hiyo. Sisi watu wazima hatutaweza. Pia sisi huwa tunatuma message au kupiga mara 2 tu kwa siku. Asubuhi na jioni. Sio kila mara kuchat hovyo.

Kimsingi binti mwenye umri mkubwa achana na mambo ya kutaka attention kama binti wa miaka 22. Wewe muda wako ushapita.
 
Wewe MamaSamia2025 usituongelee Wanaume, hatujakutuma. Ukitaka kuongea na wanawake wenzako nendeni hukon kwenye kitchen galla
 
Lorch
 
ungemshauri huyo uliyemweka jina lako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…