Kwa binti mwenye umri mkubwa acha hizi tabia unapompata mwanaume mwenye nia ya kukuoa

Kwa binti mwenye umri mkubwa acha hizi tabia unapompata mwanaume mwenye nia ya kukuoa

Kudekezana na hizo za kuulizana ulizana nionavyo hata hazina umri bali ni jinsi tu mtakavyo kuwa mmejizowesha na huyo mtu mzima mwenzako toka mwanzo.

Mkijizowesha kuwasiliana mara mbili kama dawa za asubuhi na jioni basi mtaendelea vivyo hivyo na mkijizowesha kuwasiliana kila nafasi inapopatikana kwa kuulizana umekula, kupeana pole hiyo pia inaendelea siku zote.
 
Naongea na mabinti wa miaka 35 au zaidi. Huu umri kama upo single ni mkubwa kwa mwanadada hivyo kuna mambo lazima ukubaliane nayo kuwa hayapo upande wako kwa sasa. Ukishupaza shingo shauri yako.

Endapo umepata mwanaume aliye tayari kukuoa mwenye umri kukuzidi lazima ukubali kuwa hakutakuwa na mambo kama ya wapenzi wenye umri mdogo (under 30s).

Mtu mwenye umri huo hawezi kuwa na mambo ya kukutumia message za umekula? Umevaa nini? Au zingine za kitoto. Vinginevyo utafute Mario mwenye umri mdogo ili akupe attention za namna hiyo. Sisi watu wazima hatutaweza. Pia sisi huwa tunatuma message au kupiga mara 2 tu kwa siku. Asubuhi na jioni. Sio kila mara kuchat hovyo.

Kimsingi binti mwenye umri mkubwa achana na mambo ya kutaka attention kama binti wa miaka 22. Wewe muda wako ushapita.
Single mother again
 
Jezi namba 35 -40 zinahitaji wavae wataalamu na sio vijana wadogo manaa zinavaliwa kitaalamu na zinahitaji hekima Sana
 
Kudekezana na hizo za kuulizana ulizana nionavyo hata hazina umri bali ni jinsi tu mtakavyo kuwa mmejizowesha na huyo mtu mzima mwenzako toka mwanzo.

Mkijizowesha kuwasiliana mara mbili kama dawa za asubuhi na jioni basi mtaendelea vivyo hivyo na mkijizowesha kuwasiliana kila nafasi inapopatikana kwa kuulizana umekula, kupeana pole hiyo pia inaendelea siku zote.
Ila kisaikolojia wanasema women , wanahitaji attention Kama kupigwa pigiwa phone , messages n.k

Sasa mtoa mada si atakuwa anaenda against the nature of women , maana hata ile kutongozwa mwanamke nasikia anafurahia.
 
Kweli kabisa usemalo Mkuu.

Mleta uzi yampasa alijue hili kuwa umri kwenda sio tatizo hata.
 
Back
Top Bottom