Kwa CCM hii, Maendeleo ya kweli kama Taifa tusahau milele

Kwa CCM hii, Maendeleo ya kweli kama Taifa tusahau milele

mockers

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
12,843
Reaction score
35,442
Hivi hiki chama mnakielewa kina falasafa ipi ya kueleweka.

Ukiitafsiri CCM ilivyo ukiwa umetulia kabisa utaona kua haitokuja kutokea CCM ilete maendeleo hata siku moja,
Rushwa iliyokithiri ni kansa kubwa inayosababishwa na CCM.

Hata watumishi wa umma kama walimu, manesi, maafisa kilimo, polisi wanalipwa mishahara wasiyostahili, na hawapewi stahiki zao kwa sababu CCM wanaongoza kutapanya pesa za nchi hii.

Hawana tena mipango ya maendeleo yaani kila kitu wameshashindwa, elimu bora hakuna, kwenye utalii wako hoi, ulinzi wa rasilimali ndio basi tena wanagawa tu bila kuangalia kesho ya wajukuu wetu itakuaje na vizazi vijavyo itakuaje.

Hivi mtu mwenye akili timamu hawa jamaa mnawaelewa kweli
 
CCM ni chama tapeli. Viongozi wake wengi wanafanya siasa za kitapeli, na hivyo hurithisha huo utapeli mpaka kwa Serikali yake.

Ukitizama siasa za CCM na mipango ya Serikali ya CCM, ukalinganisha na mataifa mengi yaliyofanikiwa, utaona wazi kabisa CCM na Serikali yake ipo kwaajili ya kuwafukarisha wananchi. Na hayo inafanya kupitia sera zake mbaya za kodi na sera hovyo za maendeleo.

Duniani kote, kanuni ya kodi ni kuwa huwezi kutoza kodi zaidi ya mara moja kwa mapato yale yale, lakini Serikali ya CCM inaweza kutoza kodi zaidi ya 10, kwa mapato yale yale, kwa kubadilisha majina ya kodi. Wapo tayari kumtoza kodi bibi kizee asiye na kipato huko kijijini kwa kununua vocha ya simu ya sh 500, ili tu ipatikane pesa ya wakubwa wa Serikali kuzurura nje ya nchi na makundi ya wasanii wanaolipiwa malazi na chakula, na kupewa pesa ya kufanyia starehe sh 2,700,000 ($1,000) kwa siku!!

HIYO NDIYO CCM, adui mkubwa wa ustawi wa Watanzania.
 
Imagine uchaguzi wa mwakani watakuja na ahadi za tutawaletea maji, tutawaletea madawati, tutawatengenezea barabara...

Miaka zaidi ya 60 madaraka vitu basics tu wameshindwa. Kuna kurusha setilaiti kweli chini ya CCM?

CCM uwezo wake umeishia hapo.
 
Back
Top Bottom