Kwa CCM mnaoratibu mipango ya Maandamano Rais aongezewe muda, kumbukeni na haya.

Kwa CCM mnaoratibu mipango ya Maandamano Rais aongezewe muda, kumbukeni na haya.

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Wanaccm mnaoratibu mipango ya kufanya maandamano ili Rais aongozewe muda wa kusalia madarakani kumbukeni na haya, muwe makini msije mkachafua hali ya hewa tukatafutana.

1.Mnakumbuka kwamba kumekua na matamanio ya baadhi ya wanasiasa, viongozi wa dini na wanaharakati kadhaa kutaka kuitisha maandamano ya amani kudai Katiba mpya? Mkiitisha na wao wataitisha ya kwao

2.Hao Polisi wa kutoa kibali watatoka nchi gani wakati walishazuia yale ya kudai katiba mpya wakidai masuala ya kisheria yana taratibu zake na siyo kuandamana?

3.Mkumbuke kua Rais alishasema kwamba yeye hatoongeza muda hata dakika moja, kwanini mnataka kuichafua sifa ya kiongozi wetu wa nchi? Mnataka kumlazimisha ili iweje?

4.Muelewe akiongezewa muda na wengine nao watadai waongezewe muda baadae, hamuoni kua mnatengeneza ***** ***** mpya za kuharibu amani ya nchi yetu?
 
Subiri tuone maana mtoto akililia wembe mpe umkate
 
Mkuu! Chini ya Mbawa za CCM uliyosema yote hayana mantiki!

Na usiamini kabisa kitu akitamka mwanasiasa kwamba sitoongeza muda, refer to Dkt Bashiru kwamba hatokubali uteuzi wowote!

Wanasiasa ni waongo sana, issue iko hivi; Ni kwamba jamaa atatawala daima milele(atafia madarakani), Kikubwa ni kujiandaa kisaikolojia, usishupaze shingo,itavunjuka.

Ni busara kucheza kwaito kama inayopigwa ni kwaito, usicheze kihindi kwenye mdundo Wa reggae!

Family First! Mengine tuyaache redioni.
 
Kunayo haja ya wanachama baadhi kupimwa afya ya akili, huwezi amini hata darasa la 7 haimwingi akilini
 
Kwa ufahamu wangu ni kwamba kiongozi huyu ataongeza muda sina taabu kktk hili na yeye mwenyewe ndiye anaeratibu hili nilisha jipanga siku nyiingi na hao wanaoshadadia madaraka ya milele wakisha maliza kazi yao watafurumushwa na huyo walemteua na kisha woote bila kujali rangi, dini wala vyama tutaungana woote kumuondoa.
 
Hakuna mwana ccm anaefanya uratibu wa hayo maandamano bali ni vichaa flani wanataka kuleta tafrani na kichaa kisheria ni mtu asiyejitambua hana madhara hivyo msijali
 
Tunaandama msitutishe tunataka rais wetu mpendwa aongezewe mda ili inchi yetu izidi kupaa, china wameweza sisi tushindwe tuna nini.
 
Kwa ufahamu wangu ni kwamba kiongozi huyu ataongeza muda sina taabu kktk hili na yeye mwenyewe ndiye anaeratibu hili nilisha jipanga siku nyiingi na hao wanaoshadadia madaraka ya milele wakisha maliza kazi yao watafurumushwa na huyo walemteua na kisha woote bila kujali rangi, dini wala vyama tutaungana woote kumuondoa.
Wanatumika kama kondomu kisha wanatupwa wanakuja ungana na Jamii hio hio iliyopinga hayo.wapo wapi hawa chawa Bashite, nkamia, Kessy,musiba, lugola mbona awaimbi tena chorus baada ya shibe kukoma.Mtu mweusi ni duni Sana kwenye kujikomboa kifikra.
 
Tunaandama msitutishe tunataka rais wetu mpendwa aongezewe mda ili inchi yetu izidi kupaa, china wameweza sisi tushindwe tuna nini.
China ya nini tena jaman si tulikubaliana hatupangiwi wala hatuigi mtu yyte.

Anyway We’re All Set, Tukutane Ulingoni
 
Tunaandama msitutishe tunataka rais wetu mpendwa aongezewe mda ili inchi yetu izidi kupaa, china wameweza sisi tushindwe tuna nini.
Kipi cha maana alichofanya.China ni sahihi sababu ameiunua maisha ya wachini na sio kugusa chawa wachache huku wanyonge wakinyongeka.
 
Hakuna Cha kumzuia Magufuli kua Raisi mpaka 2040 muda utaongea
Swali langu ni moja tu wenzie walio muachia madaraka wangekuwa na tamaa kama zake yeye angepata nafasi hiyo anayo itaka kuing'ang'ania? Hivi huyu ndiye anajihubiria kila siku kuwa ni mzalendo? Uzalendo ni kuratibu mipango ya kubaki madarakani?
 
Back
Top Bottom