Kwa CV hii ya Msigwa! Je, ni eligible kuweza kusimamia maliasili na utalii??

Kwa CV hii ya Msigwa! Je, ni eligible kuweza kusimamia maliasili na utalii??

Status
Not open for further replies.

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,149
Reaction score
3,825
WanaJF!

Hapa nchini Tanzania kuna sekta fulani fulani ambazo ni nyeti na zinapaswa kupewa uangalizi wa kina ili ziweze kuleta tija kwa taifa. Mfano tu wa sekta hizo ni sekta ya maliasili na utalii, sekta hii kama ikiweza kusimamiwa vizuri, sio tu itaipatia serikali mapato yake, bali itaweza vile vile kuitangaza nchi yetu kote duniani ili ulimwengu uweze kuitambua Tanzania.

Sasa katika suala zima la kuisimamia hii sekta, na kwa kasi ambayo CHADEMA wanayo katika kutwaa dola, ni vyema kama wananchi tukijadili uwezo wa watu wanaopewa dhamana katika usimamizi wa sekta zetu, kwani wote tunafahamu umuhimu wa raslimali watu katika kusukuma gurudumu la maendeleo kokote pale duniani.

Leo namleta kwenu Mhe Msigwa ambae ni mbunge wa jimbo la Iringa mjini na pia ni waziri kivuli wa maliasili na utalii, lakini pia mchungaji Msigwa ndiye anae tarajiwa kupewa dhamana ya kuongoza wizara hii nyeti ya maliasili na utalii endapo CHADEMA itatwaa dola, sasa kwa CV yake ndugu Msigwa na majukumu anayo tarajiwa kukabidhiwa, sidhani kama kweli atamudu katika utendaji.

kwani huu umaarufu alioupata wa kuropoka kuwa Kinana ni jangili sio kigezo toshelezi kusema Mchungaji Msigwa ni mtu sahihi kwenye sekta ya maliasili na utalii, CHADEMA tupeni mtu mwingine Msigwa ni mwepesi mno!!

CV ya mchungaji Msigwa ni hii hapa;

Msigwa.PNG
 
kuhusu kinana kwenda kumshitaki msigwa imeishia wapi inaaonekana wabunge wa wanawasumbua mmeshaanza kuogopa kabla hatufika 2015 mtafurahi
 
Hivi kwanini wabunge wengi wa CHADEMA hawana shahada?

Hivi tungesema leo kwenye katiba mpya wabunge angalau wawe na shahada hawa wabunge wa CHADEMA wangechomokea wapi?

Angalizo; Elimu ni muhimu na ndio maana watoto wetu wakipata sifuri tunailaumu serikali! na hatutaki hao walio pata sifuri watuongozee nchi yetu.
 
Kwa taarifa kama CDM itachukua nchi, vyeo havitakuwa vya kupeana kama ilivyo sasa na serikali ya magamba. Mawaziri hawatakuwa wanasiasa bali wataalamu wa maeneo husika. Nafasi zote za juu kuanzia uwaziri zitatangazwa na watu watatakiwa ku apply na watafanyiwa interview ili kupata mtu stahiki kwa nafasi sahihi.
 
Wewe ndiye msemaji wa chama? maana ni juzi tu hapa Wenje amelitangaza baraza la mawaziri akiwa huko Mwanza. Mawaziri matakuwa hawa hawa, kwa kuongezea tu, Lema waziri wa mambo ya ndani!
 
ina dhihirisha jinsi ulivyo mfinyu wa akili leta mada yenye maana ya kujenga nchi acha majungu
 
ina dhihirisha jinsi ulivyo mfinyu wa akili leta mada yenye maana ya kujenga nchi acha majungu

Wewe kilaza mbona mgumu kuelewa? mleta mada amesema waziwazi umuhimu wa raslimali watu katika kusukuma gurudumu la maendeleo, hivyo tuanze kujadili hao watu wenyewe kabla ya kuwapa fursa!
 
msigwa nyerereism ypo kwa maslai ya wakatoriki

Wakatoliki wanakuumiza sana kichwa, CV hapo juu ya msigwa imeonyesha kua yeye ni mchungaji na coordinator wa vine yard church hapa nchini sasa Wakatoliki wametoka wapo hapo?
Msigwa ni mchungaji na ana kanisa lake ambalo ni Vineyard
 
Wewe ndiye msemaji wa chama? maana ni juzi tu hapa Wenje amelitangaza baraza la mawaziri akiwa huko Mwanza. Mawaziri matakuwa hawa hawa, kwa kuongezea tu, Lema waziri wa mambo ya ndani!

Na huyo unayesema alitangaza baraza la mawaziri ni msemaji wa chama...?
 
Hivi hao wenye shahada wamelifanyia nini taifa? Mbona ndo mafisadi wakubwa wa rasilimali zetu? Ccm yote imejaa wapumbavu!
 
Cdm utaipenda tu,magamba wameanza kuja na hoja chakavu.
 
Wewe kilaza mbona mgumu kuelewa? mleta mada amesema waziwazi umuhimu wa raslimali watu katika kusukuma gurudumu la maendeleo, hivyo tuanze kujadili hao watu wenyewe kabla ya kuwapa fursa!

Kwenye kuisaka dola hakuna elimu ndugu mwana CCM....ila kwenye kuendesha dola yes....Watu wa kufanya hivo wapo wengi tu...........hebu angalia katika baraza hili la kwanza la Tanganyika na unionyeshe wale waasisi wa kupigania uhuru wako wangapi?
Yu wapi BIBI TITI.....SAADAN KANDORO......AKINA SYKES?

wpfd728139_05.jpg
 
Wakatoliki wanakuumiza sana kichwa, CV hapo juu ya msigwa imeonyesha kua yeye ni mchungaji na coordinator wa vine yard church hapa nchini sasa Wakatoliki wametoka wapo hapo?
Msigwa ni mchungaji na ana kanisa lake ambalo ni Vineyard

mkuu jamaa mpuuzi,huna budi kumpuuzia.
 
WanaJF!

Hapa nchini Tanzania kuna sekta fulani fulani ambazo ni nyeti na zinapaswa kupewa uangalizi wa kina ili ziweze kuleta tija kwa taifa. Mfano tu wa sekta hizo ni sekta ya maliasili na utalii, sekta hii kama ikiweza kusimamiwa vizuri, sio tu itaipatia serikali mapato yake, bali itaweza vile vile kuitangaza nchi yetu kote duniani ili ulimwengu uweze kuitambua Tanzania.

Sasa katika suala zima la kuisimamia hii sekta, na kwa kasi ambayo CHADEMA wanayo katika kutwaa dola, ni vyema kama wananchi tukijadili uwezo wa watu wanaopewa dhamana katika usimamizi wa sekta zetu, kwani wote tunafahamu umuhimu wa raslimali watu katika kusukuma gurudumu la maendeleo kokote pale duniani.

Leo namleta kwenu Mhe Msigwa ambae ni mbunge wa jimbo la Iringa mjini na pia ni waziri kivuli wa maliasili na utalii, lakini pia mchungaji Msigwa ndiye anae tarajiwa kupewa dhamana ya kuongoza wizara hii nyeti ya maliasili na utalii endapo CHADEMA itatwaa dola, sasa kwa CV yake ndugu Msigwa na majukumu anayo tarajiwa kukabidhiwa, sidhani kama kweli atamudu katika utendaji.

kwani huu umaarufu alioupata wa kuropoka kuwa Kinana ni jangili sio kigezo toshelezi kusema Mchungaji Msigwa ni mtu sahihi kwenye sekta ya maliasili na utalii, CHADEMA tupeni mtu mwingine Msigwa ni mwepesi mno!!

CV ya mchungaji Msigwa ni hii hapa;

School Name/Location Course/Degree/Award
All Africa Bible College, South Africa
Sangu Secondary School
Magoye Primary School

[TH="align: center"] Start Date [/TH]
[TH="width: 13%, align: center"] End Date [/TH]
[TH="width: 10%, align: center"] Level [/TH]

[TD="align: center"]B.Ministry[/TD]
[TD="align: center"]1999[/TD]
[TD="align: center"]2004[/TD]
[TD="align: center"]GRADUATE[/TD]

[TD="align: center"]O-Level Education[/TD]
[TD="align: center"]1983[/TD]
[TD="align: center"]1986[/TD]
[TD="align: center"]SECONDARY[/TD]

[TD="align: center"]Primary Education[/TD]
[TD="align: center"]1976[/TD]
[TD="align: center"]1982[/TD]
[TD="align: center"]PRIMARY[/TD]
Company Name
The Parliament of TanzaniaMember - Iringa Urban Constituency
Vineyard ChurchNational Coordinator

[TH="colspan: 4, align: left"] EMPLOYMENT HISTORY [/TH]

[TH="align: center"] Position [/TH]
[TH="align: center"] From [/TH]
[TH="align: center"] To [/TH]

[TD="align: center"]2010[/TD]
[TD="align: center"]2015[/TD]

[TD="align: center"]2005[/TD]
[TD="align: center"]2010[/TD]

Kama CV ndio kuwa na uhalali wa kuwa kiongozi bora, naamini Tanzania isinge kuwa hapa ilipo. Jiulize ni Mawaziri wangapi wa MAGAMBA wenye elimu kubwa walio iongoza hiyo Wizara na hatimaye tumefika hapa tulipo!!??

Jiulize ni wasomi wangapi walio toa mapovu bungeni kutetea wizi na uporaji wa Maliasili kisa Msigwa kamtaja mkuu wa MAJANGILI TZ huku akitumia vyombo vyake kusafirisha nyara zetu!!!

Si umeona walio soma lakini hawakuelimika na hatimaye kuto fahamu KATIBA ya nchi inasema nini kuhusu haki ya kuishi ya kila mTanganyika, na kujikuta waki bwatuka hovyo Bungeni wakati ni viongozi wakuu??

BURE KABISA NA CV zako!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom