Kwa dhati kabisa tunalipongeza sana jeshi la polisi ila na wao tutawalaumu pia naamini kabisa mnyororo wa watuhumiwa haujaisha

Kwa dhati kabisa tunalipongeza sana jeshi la polisi ila na wao tutawalaumu pia naamini kabisa mnyororo wa watuhumiwa haujaisha

Mkwawe

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2016
Posts
3,132
Reaction score
5,508
Kwa uelewa wangu mdogo huyu "msaidizi wa paroko" hajakurupuka kuanzisha hii misheni lazima Kuna soko ambalo amelilenga na hiki kivuli cha usaidizi wa paroko ni moja ya kukamilisha misheni chafu ambazo naamini nyingi amekwishazitekeleza na hii imembumia kwa kuwa watanzania walilisimamia kidete hili jambo na kulipazia sauti

Mtoto amepotea mei 30 na taarifa ghafla ikasambaa kwa mamlaka za mkoa wa Kagera na wilaya ya muleba, wiki mbili na siku kadhaa mtoto hakupatikana amekuja kupatika akiwa mauti na baadhi ya viungo vyake kunyofolewa na siku moja tu baada ya kupatikana maiti na saa kadhaa watuhumiwa takribani tisa wanakamatwa wakiwa na viungo vya mtoto...

Hapa ndo Mimi napatwa na ukakasi wiki mbili tangu mtoto apotee inaonesha wazi alikuwa hai mahali fulani lakini mtoto hakupatikana kwanini muda mfupi tu baada ya mtoto kufariki ndo iwe rahisi kuwapata watuhumiwa? Je ni rahisi sana kupata viungo vya mtoto kuliko mtoto mwenyewe?

Hapa Kuna hujuma kubwa sana inazunguka na ndiyo maana nasema huu mnyororo haujaisha kwa msaidizi wa paroko tu na genge lake Kuna watu inaweza ni wa system pia wanahusika

Nalipongeza jeshi la polisi ila hii kesi bado kabisa Kuna nguvu kubwa iko juu ya hili pengine inaweza kuwa baadhi ya watu wa system nao hujifanya wanadhughulikia hii kesi ila ni wahusika maana haya matukio mara nyingi hutokea nyakati za uchaguzi Sasa hapa Kuna kitu, mwaka huu ni uchaguzi na mwakani pia...

KRISTU TUMAINI LETU

PIA SOMA
- Kifo cha Asimwe Novath (Albino); Baba mzazi na Paroko msaidizi washikiliwa kwa tuhuma za mauaji

- Update: Mwili wa Mtoto Albino (Asimwe) wakutwa hauna baadhi ya viungo
 
Mkuu, hadi huo mwili kupatikana usikute mambo yalikuwa yamekwiva huko kwa ground,
Kupatikana kwa mwili na viungo hivyo sio emergency, ni kazi watu wamefanya kwa muda mrefu
 
Mkuu, hadi huo mwili kupatikana usikute mambo yalikuwa yamekwiva huko kwa ground,
Kupatikana kwa mwili na viungo hivyo sio emergency, ni kazi watu wamefanya kwa muda mrefu
Nafikiri pia imechochewa na kauli ya rais kusema kua mauaji haya yamemsikitisha sana,ile kauli ni kama amri kua uchunguzi ufanyike haraka sana na watuhumiwa wakamatwe.
 
Mkuu, hadi huo mwili kupatikana usikute mambo yalikuwa yamekwiva huko kwa ground,
Kupatikana kwa mwili na viungo hivyo sio emergency, ni kazi watu wamefanya kwa muda mrefu
Kaka huu msemo "Serikali ina mkono mrefu" haiko kwa bahati mbaya
Uwezekano wa kuokoa maisha ya mtoto ulikuwa mkubwa sana ila naamini Kuna wakubwa wanahusika, hakika naamini hivyo
 
Nafikiri pia imechochewa na kauli ya rais kusema kua mauaji haya yamemsikitisha sana,ile kauli ni kama amri kua uchunguzi ufanyike haraka sana na watuhumiwa wakamatwe.
Haki ya Mungu hiki kifo ni kama kilipangwa, nimeumia sana yaani mtoto mzuri sana halafu watu wamemkatakata kama vipande vya supu
 
Serikali ikiamua kushughulikia jambo serious chap tu inalitatua. Shida huwa ni kuamua. Na hiyo shida mara nyingine huchangiwa na wahusika kuwa sehemu ya mfumo.
 
Serikali ikiamua kushughulikia jambo serious chap tu inalitatua. Shida huwa ni kuamua. Na hiyo shida mara nyingine huchangiwa na wahusika kuwa sehemu ya mfumo.
Hii serikali katili sana yaani daah ni ngumu sana mtu wa kawaida aamue tu kujiulia albino na ikiwa trend ya makosa haya inajulikana kabisa
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Hata wakitajwa wakiwa na fedha..... Zip, wataumia hao hao. Ina maana hivi viungo walivitafuta wakiwa hawana mteja? Na kama walikuwa naye, kwa nini viungo wanavyo wao?
Halafu kwanini mtoto asipatikane ndani ya wiki tatu kasoro ila viungo vipatikane ndani ya siku moja baada ya kifo
 
Hao washika pingu waliambiwa mtoto kapotea, sasa sijui na wao walikuwa na baba Mtumishi ndo wakatulia, mpaka Mheshimiwa alipotoa machozi ndo wakajishtukia?

Ama sivyo waseme tu nini kiliwakumba
 
Hao washika pingu waliambiwa mtoto kapotea, sasa sijui na wao walikuwa na baba Mtumishi ndo wakatulia, mpaka Mheshimiwa alipotoa machozi ndo wakajishtukia?

Ama sivyo waseme tu nini kiliwakumba
Madam Shangaa na wewe!
Na hata huyo mheshimiwa nahisi aliona aibu baada ya trend ya hii habari kushika hatamu kwenye media nyingi
 
Kaka huu msemo "Serikali ina mkono mrefu" haiko kwa bahati mbaya
Uwezekano wa kuokoa maisha ya mtoto ulikuwa mkubwa sana ila naamini Kuna wakubwa wanahusika, hakika naamini hivyo
Uko na point fulani.
Serikali haiwezi kushindwa kumkamata muhalifu ambaye yuko ndani ya nchi na ndani ya mkoa huohuo aliofanyia uhalifu labda ukimbilie Burundi hapo kidogo utawaumiza kichwa.
 
Uko na point fulani.
Serikali haiwezi kushindwa kumkamata muhalifu ambaye yuko ndani ya nchi na ndani ya mkoa huohuo aliofanyia uhalifu labda ukimbilie Burundi hapo kidogo utawaumiza kichwa.
Jumba bovu limekuangukia msaidizi
 
Uko na point fulani.
Serikali haiwezi kushindwa kumkamata muhalifu ambaye yuko ndani ya nchi na ndani ya mkoa huohuo aliofanyia uhalifu labda ukimbilie Burundi hapo kidogo utawaumiza kichwa.
Jumba bovu limemuangukia msaidizi
 
Back
Top Bottom