Kwa Dkt. Dorothy Gwajima, CCM imelamba Dume. 2025 Rais awe yeye kulingana na usomi alio nao

Kwa Dkt. Dorothy Gwajima, CCM imelamba Dume. 2025 Rais awe yeye kulingana na usomi alio nao

Sio Vema kumuangalia kwa jinsia yake ..., anaweza kuangaliwa kwa kigezo kingine ...mfano rais wa sasa anatoka "Chato" sio lazima rais anayekuja bado atoke Chato kwani hii ni nchi kubwa ...
Utasemaje ccm imelamba dume wakati ni jike?!!
 
Huyu ndio atakuwa Waziri wa Kwanza Kutumbuliwa.

Wizara ya Afya haitaki Waziri alie Somea mambo ya Afyaa Lazima Atapishana na Muheshimiwa
I can bet with you kwa kiwango chochote na nikakushinda. Dr Dorothy Gwajima ni kati ya Mawaziri watakao maliza hadi 2025 na Rais wa Awamu ya 5 wakisimamia afya.

Tofauti ya Waziri huyu na waliotangulia ni kwamba licha ya Kwamba kapitia nafasi nyingi kwenye sekta ya afya kama kuwa Daktari hospitalin, DMO, RMO, DCS Wizara ya Afya na Naibu KM- TAMISEMI bado ana UBUNIFU wake na DELIVERABLES zake ambazo Ali achieve na zinaishi mpaka sasa. Ni mchapa kazi, mkweli na mwaminifu

Anayesubiri Dr Gwajima afeli atasubiri sana
 
Sio udini ni maelewano.
Nyerere mwinyi
Mkapa jk
Magu kasim
Acha ujinga ww! Haturudi tena egypt! Ndege yetu inatakiwa iendelee kupaaa! Kasim achape kazi na wala asiwaze irais! Udini ktk urais umetirudisha nyuma saana Tz! Rais mwenye vigezo bila kujali dini yake na jinsia yake! Kwa sasa kigezo ni kuwa mzalendo kama au zaidi ya Magufuli!
 
Sema huyu mama kauzu sana..ila anafanya kazi! Pongezi kwake.
 
Nampendekeza kwenu Bi Dorothy

Itakuchukua muda mfupi sana baada ya kumtazama katika utekelezaji wa majukumu yake Bi. Dorothy kutambua kipawa alicho nacho cha uongozi, nimemsikiliza katika clip inayosambaa akifanya analysis na wadau katika wizara aliyokuwa akihudumu kama Naibu Katibu Mkuu, kikweli CCM msifanye ajizi anzeni sasa kumuandaa na huyu ndie atakuja kuwa Rais wetu baada Dr. Magufuli
Mnafikiria madaka tu na siyo maendeleo na maisha ya watu!!!
Ccm ni zimwi
 
Personally namuona kama muigizaji na sio kiongozi. Kiongozi bora ni yule ambaye matokeo yanaonekana bila kamera. Huyu anaongozana na waandishi wa habari hata akimuhoji mtu anataka wawe wana-shoot. Sioni kama atafika mbali. Kiongozi kama Mh. Lukuvi ambaye mpk tunapigiwa simu tufuate hati wakati tulishakamilisha mchakato toka awamu ya pili ndiye naweza kusema anachapa kazi sio kufanya kazi kwenye makamera bila matokeo
 
Nampendekeza kwenu Bi Dorothy

Itakuchukua muda mfupi sana baada ya kumtazama katika utekelezaji wa majukumu yake Bi. Dorothy kutambua kipawa alicho nacho cha uongozi, nimemsikiliza katika clip inayosambaa akifanya analysis na wadau katika wizara aliyokuwa akihudumu kama Naibu Katibu Mkuu, kikweli CCM msifanye ajizi anzeni sasa kumuandaa na huyu ndie atakuja kuwa Rais wetu baada Dr. Magufuli
Ebu acha ujinga huo, Urahisi haupatikani hivyo, na sana sana unaweza kumuharibia, kuna January Speech write wa Raisi, na kusomea USA, etc kadhalika alishindwa kufikia huko, kuna 1st Class ya Economics, naye alishindwa kufikia huko, kuna Marehemu Dr William alishindwa, na kama kigezo ni elimu basi ili tuwe fair kwa wengine mwaka 2024 tunaanza kuwafanyia mitihani ili kufikia 2025 April tuwe tumepata majina wala 3 .
Karibu tena
 
Hakuna msomi atakayetumia elimu yake katika utawala huu ,kuna wasomi walijaribu wakaishia kutumbuliwa....Hao walioteuliwa ni kwa ajili ya kupokea maelekezo kutoka kwa jeshi la mtu mmoja.
Ni mtihani kweli kweli Kati ya kutumia usomi wako au kutii maagizo usife njaa
 
Dorothy ni kiongozi mzuri tena sana kama atajikita sana kwenye kupigania uhai na maisha ya watu maskini. Anahitaji sana kumuomba Mungu ampe hekima ili aweze kufanya maamuzi yenye kuleta matumaini kwa wengi. Nasema hivi kwa sababu viongozi wengi wakishapata teuzi wanaamini sana katika mamlaka na nguvu ya cheo chake kuliko watu ambao ndiyo chanzo cha nguvu hiyo.
 
Kajambo kamoja ulikomwona anakafanya tayari akili imekimbilia urais!!
Amakweli nchi wajinga niwengi
 
Mwanamke for President!I am sorry,mwananke hapaswi kumuongoza mwanamna.That is Biblical.Nipigeni madongo na mawe,lakini huo utabaki kuwa ukweli,sitapepesa macho ng'o.We man were created to be leaders,not women.Hii dhana ya wanawake kuongoza wanaume imetoka kuzimu jamani,tuwe makini.

Kwa bahati mbaya sisi bila kujua tumeikumbatia.Halafu mianaume mingine nayo,noma sana, bila aibu inaipigia chapuo.Sijui imelambishwa nini na Wazungu.Shameful indeed.

NGOs hizi zinatuletea vitu vya ajabu sana,mara mfumo dume,mara tohara kwa wanaume,aibu tupu.Mfume dume ndio mnyama gani?
Kwa hiyo mkuu una govi[emoji124][emoji124][emoji124]
 
Hukusikia hotuba ya rais siku anawaapisha nawaziri kabudi na mpango, alimsifia sumaye kuvunja rekodi ya miaka 10 ktk uwaziri mkuu!! Hii ilikuwa meseji sent kuwa kasim majariwa nae atavunja rekodi ya waziri mkuu kuwa rais.

Over.
Pamoja na "MATAGA" wa marekani kuandamana wakitaka bwana "TRUMP" asalie madarakani pamoja na kushindwa, ila hujasikia IGP wakule akisema watapigwa kipigo cha mbwa koko, makamo wa raisi Mike Pence yani mama Samia Suluhu Wakule kasema "MATAGA" hao wanaiaibisha MAREKANI.
Ccm na vibaraka wenu mna la kujifunza.
 
Pamoja na "MATAGA" wa marekani kuandamana wakitaka bwana "TRUMP" asalie madarakani pamoja na kushindwa, ila hujasikia IGP wakule akisema watapigwa kipigo cha mbwa koko, makamo wa raisi Mike Pence yani mama Samia Suluhu Wakule kasema "MATAGA" hao wanaiaibisha MAREKANI.
Ccm na vibaraka wenu mna la kujifunza.
Which means Chama cha Demoghasia & Maombolezo na kile cha Mr Heavy ^vinaliaibisha^ taifa letu la Tanzania, au siyo!???
 
Back
Top Bottom