Nafaka ni eneo Pana sana na limewapa mafanikio watu wengi sana (wenye mitaji mikubwa).
Nimeona mijadala mtu anasema ana mtaji wa 3million afanyaje? Wadau wanatiririka auze nafaka, sasa kwa mtaji wa million 3 na ushindani uliopo chance ya huyu kijana kutoboa iko wapi?
Let's say amepata eneo sokoni, kaenda mpanda/popote pale kwenye Michele then kabeba mzigo kwa mtaji wake alionao, kafikisha sokoni ili upate faida ya 10,000/= inabidi huyu jamaa auze gunia loote, ni mazingira machache sana ambayo kwa anayeanza kwa kupima kwa kilo kuuza gunia lote kwa rejareja, hipi ni nafasi ya huyu kijana kukua?
Mliofanya nafaka mlianza kufanya kwa mbinu gani mpaka mitaji ikakua?