Kwa first year na wanachuo wote

mwanangu nimemwambia asome political science awe kama John Mnyika mwanasiasa halafu bungeni atoe hoja ya makandarasi kanjanja na wewe ukiwemo.
Nani mshindi hapo?

Uanasiasa sio lazima usomee ni jinsi utakavyoweza kuwavutia watu kwa uongo wako,mm sio mkandarasi kanjanja kwa sababu sijawahi kubahatisha katika elimu yote niliopitia na namshukuru M/MUNGU na namuomba anisaidie nisipate degree gamba,napenda nije nipate kidogo lakini nifurahie taaluma yangu sio kupata kingi kwa ujanja ujanja
 
kwa ardhi hamy d kidogo sikubaliani na wewe, pale karibia koz nyingi huwezi kukaa mtaan bila kitu cha kufanya ni kama pale wanaosoma COET

Afadhali umuambie na wewe.,wanadhani engineering ni sawa na degree ya insurance.
 
HAMY-D

kama wewe ni mkongwe mbona unasema mlikua mnaponda chuo pamoja na wanafunzi ISM na BAF wa ardhi wakati ISM bench ya kwanza kumaliza ni mwaka jana na BAF ni mwaka huu..umegoogle ARDHI umemjua VC wa pale ndio unajifanya unamjua sana prof mshoro..fanya utafiti usikurupuke tu..
 
Last edited by a moderator:

Sasa mkuu na wewe unabishanaje na haka kajamaa cha first year??..yani hata registration hakajafanya lakini kinaijua ardhi kuliko hata waliograduate hapo....achana naye huyuu
 
Haya wasomi wetu wa Tanzania endeleeni kutupa burudani sisi tusiofahamu hata jengo la mihadhara linavyofanana, huenda iko siku na sisi tutakua miongoni mwa wasomi.
 
HAMMY-D unatisha! Unasigina hoja kwa hoja. Tatizo unabishana na first year. Wakongwe wenzako tunakuelewa. Wala usiendelee wanafaidi bure.
 

Kama wewe unategemea google kama chanzo chako kikuu cha taarifa basi pole; ila wenzako uwa tuna shiriki vikao na hao ma-VC wa vyuo vikuu. Huyo Mshoro kabla hajawa makamu mkuu wa chuo kikuu Ardhi alikuwa ni head of department kwenye college ya Mechanics pale UDSM. Mbali na kumjua prof Mshoro kama Makamu mkuu wa chuo, pia tunafahamu maisha yake binafsi, hivyo alivyosema Prof Mshoro anaelewa hali halisi ya ajira sio kwamba alikurupuka, bali alimaanisha, na huo ndio ukweli.

Mwaka 2007 Prof Mshoro ndipo alipopitishwa kuwa makamu mkuu wa chuo kikuu Ardhi baada ya UCLAS kuwa chuo kikuu kamili kinacho jitegemea. Huku waziri mkuu mstaafu, bwana Msuya, kuwa mkuu wa chuo hicho.

Na katika transition hiyo ya kutoka kuwa university college yaani chuo kishiriki ndio zilipo anzishwa shahada mpya na actually sio mpya in such, ila ni mpya kwa majina tu, course contents zimefanywa kuchomolewa kwenye course zile kongwe na kupachikwa pachikwa kwenye hizo course mpya. Mfano course kongwe kama Archtecture imezaa interior design and landscape, Land management and valuation (LMV) imezaa REFI na PFM, Land survey imebadilishwa na kupata Geomatics na Geoinformatics, enviromental engineering imezaa enviromental science...

Kijana, ni vyema ukatumia mitandao kuuliza na kujifunza, hilo litakuwezesha kujua mambo mengi zaidi ya wenzako hapo chuo na kukufanya uwe na utambuzi mkubwa wa mambo kuhusiana na taaluma yako. Humu JF, kuna watu wengi wamesoma nje ya nchi, tena vyuo vyenye heshima tu, pia kuna watu wengi wamepita vyuo hivyo hivyo mnavyovipa hadhi kuwa ni bora, jambo la msingi ni kutumia mitandao kama huu wa jamiiforums kuweza kubadilishana uzoefu na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu mstakabali wa elimu yetu hapa nchini. Muda wa kubishana kuhusu taaluma au chuo ni bora sana na unakuwa haujaufanyia opportunity cost. Najua wengi uwa mnadanganywa na kaka zenu au rafiki zenu, ila siku zote unaambiwa, raha ya ngoma ingia uicheze mwenyewe.

Yangu ni hayo tu.
 
Vijana wengi wakitanzania hawajielewi.
Hivi unapobishana eti chuo unachosoma ni bora unataka kusema wewe ni bora na ni ubora wa kitu gani au ni nini unabishania?

Kimsingi kama chuo kina mapungufu ya resources kwa ajili ya taaluma fulani naelewa kinachofanyika either ni kuazima au kukifuata resource ilipo ili kufanikisha requirements za programmes.

watu mnabishana ujinga.

wanaobishana wenyewe chuo wanaenda kwa kuchagua degree programmes sijui nane ili abahatishe moja. huku hata chuo anabahatisha kupata kwa kujaza zaidi ya moja.

Jitambueni vijana, kwenda shule haimaanishi umeelimika.

Unaweza ukawa na PhD na bado usielimike.
someni vijana, bishaneni kwa vitu vinavyoleta positive impact katika jamii.
 
Ardhi hawatafuti kazi ila wanatafutwa wao kwa sababu ya upekee wao..sisi hatupigani vikumbo na IAA na IFM kutafuta kazi..kazi za course za ardhi bado zipo nyingi..ukitoa mifano yako naomba ARDHI uiweke pembeni..over

kama sio wewe ujue kuna wapumbumbav wengine wanafanya huo upuuzi wa kushindanisha vyuo mkuu..
 
me huwa na kwelwa sana na hii tabia ya baadh ya watu kujifany wachambuzi wa masuala ya rank za vyuo!! jaman tubadilike,naomben tutumie mda wetu vizuri sie ndio wenye dhamani ya kuleta mabadiliko ya kweli ktk taifa ambalo watu wake wengi ni tegemezi na maskini.


Ifike mahala tuuchukie umaskini na ujinga hata kwa ku~risk maisha yetu naamin sio zambi ila ni kutaka kuleta mabadiliko chanya yenye mtazamo wa kulivusha hili taifa hapa lilipo... 'it can be done,if you play your part' haya ni maneno ya muasisi wa taifa hili sote tunamfahamu(mungu amuwie radhi).

Naamin kwa dhati kabisa mabadiliko hayaji kwa usiku mmoja tu,..la hasha bali ni kwa kuwekeza ktk nyanja zote hasa elimu,.ndugu zangu naombebi tutumie fursa hii adimu ktk kupanga na kuchambua nn kizuri tunapaswa kulifanyia taifa hili kama wasomi na tunajiandaa kuwa wasomi ea elimu ya juu.

Ni mtazamo wangu jamani( pspa udom)
 
vijana mmeachana na UDINI, ss mko kwenye UCHUO hahaha nchi maskini etiii chuo gani ni bora GREAT THINKERs hawako ivyo.
 
vijana mmeachana na UDINI, ss mko kwenye UCHUO hahaha nchi maskini etiii chuo gani ni bora GREAT THINKERs hawako ivyo.

mm sijapambanisha vyuo ila imenibidi kwa sababu huwezi kuniambia degree ya insurance ifm ni sawa ba degree ya geomatics ya ARU au civil engineering ya DIT na COET
 
AgentS
Point tupu hizi na kuna wengine huwa wanakuja nimepata one kali O-level na A-level
 
Last edited by a moderator:
Nimesoma uzi huu nimejifunza kitu kimoja muhimu sana na kama tutabadilika basi nchi itaendelea maana wengi wame-base kwenye urahisi wa kupata ajira / kuajiriwa ndio kama mafanikio wamesahau wao kama wasomi wanatumiaje taaluma zao kujiajiri wengine wamekwenda mbali zaidi mpaka kuwaponda wauza nyanya wakati unaweza soma na kama ajira isipopatikana unaingia mtaani na kuuza nyanya huku ukijipanga maana usomi si kuzunguuka na bahasha ya kaki tu bali ni namna gani unatumia ela zako hata kama kidogo kuweza kuzizunguusha na ukapata nyingi, otherwise HAMY-D ameleta uzi bomba sana leo
 
Last edited by a moderator:
kwa ardhi hamy d kidogo sikubaliani na wewe, pale karibia koz nyingi huwezi kukaa mtaan bila kitu cha kufanya ni kama pale wanaosoma COET
bila shaka utakuwa upo masomoni eti "ni kama pale wanaosoma COETP".....haya bana ukimaliza kusoma 20....utatupa majibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…