Kwa gharama yoyote wapi wanatibu kiziwi na bubu kuweza kusikia na kuzungumza?

Tajirimsomi

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2017
Posts
4,824
Reaction score
5,587
Salam kwenu wadau naomba kujua wapi naweza pata hiyo tiba tumsaidie mtoto mpendwa wa jamaa yangu
 
Kuhusu ububu mkuu nafkiri kihospitali sijawai kusikia mtu katibiwa na kupona. Na pia sijui kama hata cause yake inajulikana kitabibu. Kwasabbu unakuta mtu mwingine anatoa anatoa sauti Fulani lakini hazina maana. Nafkiri hata ugugumizi pia huwa kitabibu hauleweki sana.

Au ngoja waje watalaam, jaribu rahisi ni kupitia katk maombezi nenda ktk makanisa yanayofanya maombezi atapona
 
Sawa kiongozi unamanisha hakuna tibA ya hivyo
 
Hakuna tiba ya h ivyo isipokuwa miujiza?
 
mh hapa kigugumizi huenda na jinsi taarifa zinavyo kusanywa kutafsiriwa na kutumwa kwenye viungo husika vinavyotumika kutoa taarifa hiyo(mdomo,ulimi n.k) sasa hapo kitabibu sijui kama kuna namna yoyote ya kufanya ili kuwezesha taarifa inayotaka kutolewa isiwe na mkatomkato(kigugumizi)

kwa upande wa kutokusikia vyema labda vile vifaa vya kusaidia uwezo wa kusikia. jaribu kuwaona wataalamu mkuu
 
Sawa mtaalamu ko tiba Ya moja Kwa moja hakuna
 
Isizid mil 300
sasa hiyo si mmaenda kabisa scoan na mtoto anaponywa?

kama ni bubu na kiziwi kabisa ni vya kuzaliwa navyo na YESU pekee ndo wa kumponya.huko hospital mnaenda kumtesa na ma operesheni..sindano madawa..
 
sasa hiyo si mmaenda kabisa scoan na mtoto anaponywa?

kama ni bubu na kiziwi kabisa ni vya kuzaliwa navyo na YESU pekee ndo wa kumponya.huko hospital mnaenda kumtesa na ma operesheni..sindano madawa..
Ngozi nyeusi kwa kupenda mteremko

Haha my poor Afrika
 
Sawa mtaalamu ko tiba Ya moja Kwa moja hakuna
kaka..kwa sikio kama mkitaka asikiw atafanyowa opereshen inaitwa cochlear implantation..
atapandikizwa kifaa ndani ya fuvu nyuma ya sikio..
kwa ububu sijui
 
Mkuu...kwanza Poleni na hilo tatizo naomba nikujibu kama ifuatavyo
Ububu kwanza ieleweke mtu akizaliwa hasikii tangu mtoto hawezi kuongea maana atajifunzia wapi sauti ya kile kinachotamkwa...Ila akiacha kusikia akiwa mkubwa kuongea ataweza na wapo wengi tu mtaani wa hivyo.... Ububu uliosababishwa na kutosikia hutibiwa km ataweza kusikia na kujifunza sauti...



Ukiziwi Fika Muhimbili ndio kwa Mara ya kwanza wameanza kufanya upasuaji wa kupandikiza Koklea au wanaita Cochlear Implantation ambapo atakuwa anahudhuria clinic kama madaktari watakavyo shauri na baada ya muda kidogo wataanza kuoperate Hiyo Implanted cochlear maana huwa ni programmable...

Anaweza kusikia na kuzungumza km kawaida ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…