Kwanza nianze kwa kukupongeza ni good IDEA.
Pili, ningependa kukushauri ingekuwa vizuri kama ungewasiliana na rafiki zako kwanza wa chuoni kwako, lakini kama umemalizia chuo nje ya nchi basi huna budi kufata utaratibu huu.
Tatu, kwenye kuunda hii timu yenu zingatia uhodari/ujuzi au vipawa zaidi kuliko kubeba mtu sababu ni university graduate.
Nne nakutakieni mafanikio na hii iwe mfano kwa vijana wengine wote wanaomaliza elimu ya juu, japokuwa najua si kosa lao sababu elimu ya vyuo vikuu vingi Tanzania haviwaandai vijana wetu kikamilifu kupambana katika karne hii ya 21.
Mwisho usisikilize ya watu tilia mkazo kwenye IDEA yako unless mtu aje na hard factual business/economic evidence to suggest that idea is not viable.