Kwa taarifa yako sio Magufuli wala Membe hakuna mwenye mvuto, wote wanategemea nguvu ya vyombo vya dola. Hata Lowassa angekosea ile 2015 aende chama kingine nje ya cdm, angekuwa kama Membe hivi sasa. Zito alikuwa anang'ang'ania kuungana na cdm maana anajua fika kwa huku bara, cdm ndio chama chenye wafuasi wa upinzani wa kweli. Bahati nzuri wanachama na wafuasi wa Cdm tulisema hatutaki tena taka ngumu toka ccm.
Halafu acha upotoshaji usio na tija yoyote, ccm haina wanachama 15m, kama ina wanachama wa kweli hawavuki milioni 3. Nguvu za vyombo vya dola pekee na tume isiyo huru ya uchaguzi, ndio huficha ukweli huu kuwa hadharani. Kama ccm ingekuwa na wanachama wangalau milioni tano tu hai, isingekuwa inatagemea tume ya uchaguzi kuwapitisha bila kupingwa. Cdm sidhani kama ina wanachama 1.5m, lakini ndio chama chenye wafuasi wengi hasa vijana, ila ni wasio na kadi, mfano halisi ni mimi mwenyewe. Mimi sio mwanachama wa Cdm, lakini ni shabiki wa kutupwa wa Cdm, na watu wa aina yetu ni wengi sana. Hivyo mtu yoyote akiwa ccm atategemea mbeleko ya vyombo vya dola, na akitoka asipoelekea cdm automatically anapoteza mvuto.