Hii thread yako imekaa "kisanii" kwakuwa haina mashiko isipokuwa kasumba ya itikadi ya chama.
Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ni Muungano wa Chama na wanachama wa CCM tu, haukuwa na wala hauna ridhaa ya wananchi wa pande zote za muungano, Wananchi WENGI SANA wa upande mmoja wa huo muungano wanayo malalamiko kuhusu huo muungano, sasa katika hali hiyo ni ni cha kufanya??
kwa Ule upande wenye malalamiko ifanyike kura ya maoni juu ya Muungano uwepo au usiwepo, kama wengi watasema uwepo (jambo ambalo ni impossible), basi kifuatacho ni:- aina gani ya Muungano uundwe.
Kumbuka huo Muungano ni kitu kilichoundwa na binadamu wawili (nyerere na karume) hao SIO miungu, kilichoundwa na Mungu tu kinaweza kutobadilika kuendana na wakati na haja, hivyo tusifanye huo muungano kuwa ni sheria ya Mungu isiyohitaji marekebisho au kufutwa kabisa, kumbuka binadamu ni kiumbe dynamic ni kwa sababu hiyo ndiyo maana kila uchao anapata maendeleo.
Tusiwe na mawazo mgando kuhusu huo Muungano, tuchukue hatua thabiti pale mshirika mmoja wa Muungano anapoona anadhulumiwa.
Mbona kuna nchi kadhaa zimevunja miungano yao "for the better".