Uchaguzi 2020 Kwa hali hii, CHADEMA wanajiandaa kuvunja Muungano

Uchaguzi 2020 Kwa hali hii, CHADEMA wanajiandaa kuvunja Muungano

Ujinga wa mtu mweusi, as if wazungu hawalaumiani kwenye chaguzi zao, you're just a brainwashed nyumbu.

Narudia tena, hiyo October 28 hakuna uchaguzi, bali ni kilele cha maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Sio Chadema Tanzania Bara wala ACT Wazalendo Tanzania Visiwani mwenye uwezo wa kushinda uchaguzi. Hivyo, muungano bado utaendelea kudumishwa na serikali iliyo madarakani ya CCM!
 
Hawawezi maana huu muungano tumeapa kuulinda mpaka kwa tone la mwisho la damu zetu
Ha ha ha ha... Yaani muungano unalindwa na ccm kwa kumwaga damu badala ya mapenzi ya wananchi !!!
 
Lissu yupo Zanzibar kusaka kura za urais wa Jamhuri.

Nimeanza na dibaji hiyo kwa minajili ya kusema yafuatayo:

1. Katika kunadi sera zake na ahadi za mgombea wa Urais hajawahi kuzungumzia namna atakavyolinda na kuuenzi Muungano ulioasisiwa na mababa wa mataifa ya Tanganyika na Zanzibar.

2. Akiwa Bungeni, Mhe. Lissu aliwahi kuzungumzia Muungano akionyesha kutoukubali na utayari wa kuuvunja.

3. CHADEMA katika harakati zake inakwepa kujadili Muungano wetu.

4. Hawajaweka mgombea wa urais wa Zanzibar na wametangaza kumuunga mkono Maalim Seif ambaye siku zote amekuwa akidai Muungano hauna manufaa na akiupata urais wa Zanzibar atavunja Muingano huo.

Hivyo, endapo Lissu atashinda Bara na Maalim akashinda visiwani basi meza ya muungano itapinduliwa kirahisi kifuta historia tukuka ya Muungano na mshikamano wa kitaifa.

5. CHADEMA haikutangaza awali kumuunga mkono Maalim Seif hapo awali lakini baada ya Seif kuhamasisha wafuasi wake kubeba majambia, mashoka na mundu ili kuleta machafuko, hatua hiyo imeipelekea CHADEMA kuona wamepata mshirika anayeendana na malengo yao.

Ikumbukwe CHADEMA ilipozindua kampeni zake pale Zakhiem ilitangaza maandamano ya nchi mzima kipindi hiki kwa minajili ya kushinikiza hoja zao na kuleta machafuko nchini.

Kwa sababu hii na nyinginezo inapelekea allegations za CHADEMA kujiandaa kuvunja Muungano wetu tukuka.

Hivyo, sisi wapigakura tunajua nini cha kufanya hapo Oktoba 28 ili kuulinda na kuuenzi Muungano wetu.

Msanii JF
Hataruhusiwa
 
Muungano hauna faida kwa sasa. Sanasana unawachelewesha Wazanzibari wasipige hatua kuchumi. Tunaweza kuitisha referendum ili kupata ukweli
Kwa Tanganyika muungano umeleta umaskini usio na tija. Tanganyika inabeba gharama nyingi mno
 
Kuna tofauti kubwa mno kati ya Kuvunja na Kuboresha....

Safari hii mtaelewa tu...!!
 
Haya ni matumizi mabaya ya akili. Kuzungumzia kero za Muungano siyo kuivunja bali ni kutaka kuuimarisha na Lissu siye wa kwanza kuzisema hizo kero. Semeni tu mumezidiwa hoja na hamna majibu nanyi mumezoea kujibu hoja kwa risasi.
Alishasema haufai
 
Hii thread yako imekaa "kisanii" kwakuwa haina mashiko isipokuwa kasumba ya itikadi ya chama.

Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ni Muungano wa Chama na wanachama wa CCM tu, haukuwa na wala hauna ridhaa ya wananchi wa pande zote za muungano, Wananchi WENGI SANA wa upande mmoja wa huo muungano wanayo malalamiko kuhusu huo muungano, sasa katika hali hiyo ni ni cha kufanya??

kwa Ule upande wenye malalamiko ifanyike kura ya maoni juu ya Muungano uwepo au usiwepo, kama wengi watasema uwepo (jambo ambalo ni impossible), basi kifuatacho ni:- aina gani ya Muungano uundwe.

Kumbuka huo Muungano ni kitu kilichoundwa na binadamu wawili (nyerere na karume) hao SIO miungu, kilichoundwa na Mungu tu kinaweza kutobadilika kuendana na wakati na haja, hivyo tusifanye huo muungano kuwa ni sheria ya Mungu isiyohitaji marekebisho au kufutwa kabisa, kumbuka binadamu ni kiumbe dynamic ni kwa sababu hiyo ndiyo maana kila uchao anapata maendeleo.

Tusiwe na mawazo mgando kuhusu huo Muungano, tuchukue hatua thabiti pale mshirika mmoja wa Muungano anapoona anadhulumiwa.

Mbona kuna nchi kadhaa zimevunja miungano yao "for the better".
Mabunge yaliridhia
 
Wazanzibar wanaona kama kuvunja muungano ni neema kwao Ila unapotatua tatizo linaibuka tatizo je ni tatizo lipi litaibuka baada ya kuvunjika muungano?
 
Wazanzibar wapo tayari kuvunja muungano kwa kuwa hawanufaiki na muungano huu kwahiyo kuvunjika huku kutawaletea neema wao ya mataifa mbalimbali wanaoimezea mate Zanzibar kwa hiyo watapata Muungano wenye manufaa makubwa na ya haraka sana endapo watavunja Muungano Ila ndo utakuwa mwanzo wa kupotea kwa Zanzibar na Wazanzibar
 
Lissu yupo Zanzibar kusaka kura za urais wa Jamhuri.

Nimeanza na dibaji hiyo kwa minajili ya kusema yafuatayo:

1. Katika kunadi sera zake na ahadi za mgombea wa Urais hajawahi kuzungumzia namna atakavyolinda na kuuenzi Muungano ulioasisiwa na mababa wa mataifa ya Tanganyika na Zanzibar.

2. Akiwa Bungeni, Mhe. Lissu aliwahi kuzungumzia Muungano akionyesha kutoukubali na utayari wa kuuvunja.

3. CHADEMA katika harakati zake inakwepa kujadili Muungano wetu.

4. Hawajaweka mgombea wa urais wa Zanzibar na wametangaza kumuunga mkono Maalim Seif ambaye siku zote amekuwa akidai Muungano hauna manufaa na akiupata urais wa Zanzibar atavunja Muingano huo.

Hivyo, endapo Lissu atashinda Bara na Maalim akashinda visiwani basi meza ya muungano itapinduliwa kirahisi kifuta historia tukuka ya Muungano na mshikamano wa kitaifa.

5. CHADEMA haikutangaza awali kumuunga mkono Maalim Seif hapo awali lakini baada ya Seif kuhamasisha wafuasi wake kubeba majambia, mashoka na mundu ili kuleta machafuko, hatua hiyo imeipelekea CHADEMA kuona wamepata mshirika anayeendana na malengo yao.

Ikumbukwe CHADEMA ilipozindua kampeni zake pale Zakhiem ilitangaza maandamano ya nchi mzima kipindi hiki kwa minajili ya kushinikiza hoja zao na kuleta machafuko nchini.

Kwa sababu hii na nyinginezo inapelekea allegations za CHADEMA kujiandaa kuvunja Muungano wetu tukuka.

Hivyo, sisi wapigakura tunajua nini cha kufanya hapo Oktoba 28 ili kuulinda na kuuenzi Muungano wetu.

Msanii JF

Muwe mnaweka na akiba ya maneno sio kuropoka tu,, japo naombea ccm ipite lakini kwenye swala la muungano umechemsha babaa,,,hivi nikuulize swali! muungano unafaida gani kwa wazanzibari?
 
Wazanzibar wanaona kama kuvunja muungano ni neema kwao Ila unapotatua tatizo linaibuka tatizo je ni tatizo lipi litaibuka baada ya kuvunjika muungano?

Hakuna tatizo litalojitokeza isipokua wataendelea kuteseka na kupata tabu dhidi ya muungano usio na faida yoyote kwao. All in All mnahofia Oman itarudi na kuitengeneza upya zanzibar na uchumi wao utakua maradufu zaidi ya bara.
 
Back
Top Bottom