Kwa hali hii Mama huyu ana haki kudai mali?

eity 4

Senior Member
Joined
Dec 7, 2014
Posts
148
Reaction score
209
Kuna mama aliolewa na mume wake kwa ndoa ya kanisa katoliki,wakazaa na mumewe watoto wawili, then mume wake akamuacha kwao (kwa kina mwanaume) mume alipomaliza chuo hakurudi kumchukua mkewe, akaenda kuishi wilaya nyingine na mwanamke mwingine akazaa nae watoto.

Baba mkwe baada ya kujua mwanae anaishi na mwanamke mwingine akamwambia huyu mke anaweza kurudi kwao maana ni miaka mi 3 mumewe harudi na anakaa na mke mwingine, so huyu mama akaondoka, huko alikokwenda na yeye kazaa watoto 4. Hawakupeana taraka wala akukufanyika chochote kuvunja ndoa ya awali.

Ikawa mume anakaa na mwanamke mwingine ambaye wamejenga nae nyumba 2 na mashamba kadhaa. Sasa mwanaume amefariki na hakuna wosia, huyu mama (mke wa ndoa) ameenda mahakamani anataka apewe mali zote za mumewe. Yaani hizo nyumba 2 na mashamba. HIVI ANA HAKI YA KUDAI?
 
kiutaratibu ana haki...maana ni mke wa ndoa..! alitelekezwa kaja kudai haki ya watoto wake ila sasa doa..ni kwamba kazaa na mtu mwingine

kwahiyo,wakikaa wazee wataigawanya mali kwa ratio ya 65 kwa 35 wa ndoa anaanza na wa nje anafuata

haya ni maoni tu...na kila mtu ana uhuru wa maoni...
 
Kwa nini Hana haki?
Hapa nahitaji ufafanuzi wa kisheria. Kwanza je huyu ni mke halali au? Na Kama hapakuwa na talaka hiyo ndoa ilivunjikaje.
Halafu hapo mwenye tamaa nani mume aliyeoa na kumtelekeza mke kwao na watoto kwenda kuishi na mwanamke mwingine au mie?
 
Akipambana vizuri anahaki kwa ajili ya Watoto na pia ana uthibitisho wa cheti cha ndoa tofauti na huyo Mwingine ambaye mpaka Mzee anafariki amebaki na cheo cha hawara.
 
Kwa mujibu wa sheria wanandoa wanapoishi pamoja na mali zikapatikana katika kipindi hicho, hizo mali huchukuliwa kama mali za pamoja (joint assets).
Sasa inapotokea mmoja wa hao wanandoa akifariki mali za aina hiyo zote zinabakia kwa yule partner aliyebaki hai. Mali hizo hazihesabiwi katika mirathi ya marehem.
Kwa kesi ya huyo mwanamke ni wazi kua mumewe alipata hizo mali akiwa anaishi na mwanamke mwingine, hivyo ni wazi kua hapakua na mchango wa huyo mke wa ndoa ktk upatikanaji wa hizo mali, japo ndoa bado ipo sabab hakuna talaka.
Kwa mtazamo huo sasa mali za huyo marehem zikigawanywa ku mujibu wa sheria za mirathi huyo mwanamke pia atastahili share yake kama mke halali wa marehem na sio kupewa mali zote kama alivyodai.
 
eity 4 umepata jibu hapa ila hatapata chochote kile sababu akishatengana na mumewe na ameshazaa nje kisheria atapata Mari za watoto tu yeye hausiki
 
Naona haki kwani hawakuchumahawakuchuma pamoja na ndoa zilishavunjika kwani moja ya sababu ya kuvunjika ndoa ni kuwa na mahusianao nje ya ndoa na wote wamefanya hilo kwa kwende kuwa na ndoa zingine na huo muda waliokaa mbali mbali na mahusiano mengine inatosha kuvunja ndoa yao ya awali, watoto wana haki ya kupata chochote toka kwa mali alizochuma Baba yao
 
Mkuu ni vizur kutofautisha sababa zinazopelekea ndoa kuvunjika na kuvunjwa kwa ndoa.
Ni ukweli kua kwa huyo mwanamke kutengana na mumewe na kuzaa na mtu mwingine ni sabab/ ushahid kua ndoa yao ilisha vurugika kiasi cha kushindwa kurekebishika.
Lakini ni muhimu kuzingatia kua hiyo haina maana kua ndoa imevunjika kisheria. Kwa mujibu wa sheria ndoa itahesabiwa kua imevunjika pale litakapotolewa tamko la talaka na mahakama. Sasa kwa sababu katika mazingira ya huyo mama, ni wazi kua hapakua na talaka ya mahakama hivyo hadi wakat wa kifo cha huyo mumewe ndoa yao ilikua bado ikidumu.
 
Kuna mama aliolewa na mume wake kwa ndoa ya kanisa katoliki,wakazaa na mumewe watoto wawili, then mume wake akamuacha kwao (kwa kina mwanaume) mume alipomaliza chuo hakurudi kumchukua mkewe, akaenda kuishi wilaya nyingine na mwanamke mwingine akazaa nae watoto.

Baba mkwe baada ya kujua mwanae anaishi na mwanamke mwingine akamwambia huyu mke anaweza kurudi kwao maana ni miaka mi 3 mumewe harudi na anakaa na mke mwingine, so huyu mama akaondoka, huko alikokwenda na yeye kazaa watoto 4. Hawakupeana taraka wala akukufanyika chochote kuvunja ndoa ya awali.

Ikawa mume anakaa na mwanamke mwingine ambaye wamejenga nae nyumba 2 na mashamba kadhaa. Sasa mwanaume amefariki na hakuna wosia, huyu mama (mke wa ndoa) ameenda mahakamani anataka apewe mali zote za mumewe. Yaani hizo nyumba 2 na mashamba. HIVI ANA HAKI YA KUDAI?

Anayo haki zote za kupewa mali. Tena nyie wanafamilia mkifanya ujinga huyo mke mwingine anaweza kuambulia patupu.

Busara kaeni chini mkubaliane, kwanza kwamba marehemu alikuwa na wake wawili na msimamie utaratibu wa kugawa mali pasu kwa pasu la sivyo huyo mke wa ndoa ataondoka na kila kitu.

Hata kama alienda na kuzaa watoto wengine na bwana mwingine hao watoto wamezaliwa ndani ya ndoa hivyo baba yao ni yule marehemu japokuwa kisheria pia hili linaweza kuamuliwa vinginevyo
 
Mkuu ni vizur kutofautisha sababa zinazopelekea ndoa kuvunjika na kuvunjwa kwa ndoa.
Ni ukweli kua kwa huyo mwanamke kutengana na mumewe na kuzaa na mtu mwingine ni sabab/ ushahid kua ndoa yao ilisha vurugika kiasi cha kushindwa kurekebishika.
Lakini ni muhimu kuzingatia kua hiyo haina maana kua ndoa imevunjika kisheria. Kwa mujibu wa sheria ndoa itahesabiwa kua imevunjika pale litakapotolewa tamko la talaka na mahakama. Sasa kwa sababu katika mazingira ya huyo mama, ni wazi kua hapakua na talaka ya mahakama hivyo hadi wakat wa kifo cha huyo mumewe ndoa yao ilikua bado ikidumu.
Sawa ila jaribu fikiri hao wote wameenda ishi na watu wengine kwa zaidi ya miaka miwili na kwa sheria zetu mkiishi hvyo inatazamiwa kuwa ni ndoa hvyo hao wote wanandoa nyingine, hiyo ilshavunjika, kwa matendo yao hao wote wawili, kumbuka ndoa ni mkataba waweza kuwa kwa maandishi (cheti za ndoa), kwa matendo kuishi pamoja zaidi ya miaka miwili , nk vivyo hivyo kwa matendo kinyume nayo ndoa haipo
 
Hapo ni kuwa kwa "ubize" wa ndoa zao mpya walijasahua kwenda ivunja hyo, na wengeenda kwa mazingira hayo watafisiri wa sheria wangeivunjilia mbali kwa mazingira yaliyokuwepo
 
Watoto wapate shahiki zao kwa sehemu ya Marehemu Baba yao, yeye angeweza pata fidia marehemu angekuwa hai kama angemburuta mahakamani ila angewezaje sasa na ameshaolewa kwingine?
Wajuzi wa sheria watasema zaidi mimi maoni yangu ni hayo
 
Sawa ila jaribu fikiri hao wote wameenda ishi na watu wengine kwa zaidi ya miaka miwili na kwa sheria zetu mkiishi hvyo inatazamiwa kuwa ni ndoa hvyo hao wote wanandoa nyingine, hiyo ilshavunjika, kwa matendo yao hao wote wawili, kumbuka ndoa ni mkataba waweza kuwa kwa maandishi (cheti za ndoa), kwa matendo kuishi pamoja zaidi ya miaka miwili , nk vivyo hivyo kwa matendo kinyume nayo ndoa haipo
Sio kila mazingira mtu akiishi na mtu inakua ndoa.
Kisheria ndoa ya kikristo huchukuliwa kua ni ya mke mmoja, hvyo kama mtu alifunga ndoa ya kikristo hawezi kufunga ndoa nyingine mbeleni ili hali ndoa ya awali haijavunjwa kwa talaka.
So kama mtu alikaa na mtu mwingine ilikua wakifanya uzinzi tuu ila haifanyiki kua ndoa.
Pia hata ukienda ukafanikiwa kufunga ndoa kabisa bila kuvunja ndoa ya awali kwa talaka hii ndoa mpya inakua batili kabisa kwa mujibu wa sheria ya ndoa.
 
Watoto wapate shahiki zao kwa sehemu ya Marehemu Baba yao, yeye angeweza pata fidia marehemu angekuwa hai kama angemburuta mahakamani ila angewezaje sasa na ameshaolewa kwingine?
Wajuzi wa sheria watasema zaidi mimi maoni yangu ni hayo
Baada ya kutoa maoni kwenye maswaja ya kisheria ndo unakiri kua hauna ujuzi wa sheria!!?
Sio sawa kufanya hivyo mkuu, hapa kuna watu wanasoma ña wanayachukua yanayoandikwa hapa. So kama kitu hauna ufahamu nacho sio vyema sana kukizungumzia, utapotosha watu.
 
Sio kila mazingira mtu akiishi na mtu inakua ndoa.
Kisheria ndoa ya kikristo huchukuliwa kua ni ya mke mmoja, hvyo kama mtu alifunga ndoa ya kikristo hawezi kufunga ndoa nyingine mbeleni ili hali ndoa ya awali haijavunjwa kwa talaka.
So kama mtu alikaa na mtu mwingine ilikua wakifanya uzinzi tuu ila haifanyiki kua ndoa.
Pia hata ukienda ukafanikiwa kufunga ndoa kabisa bila kuvunja ndoa ya awali kwa talaka hii ndoa mpya inakua batili kabisa kwa mujibu wa sheria ya ndoa.
Huyo hapati kitu zaidi ya watoto rafiki au kwa huruma ya mke mwenzake na familia ila hana chake hapo kachuma nae nini marehemu?, ponea ponea hiyo nyumba iwe imejengwa kipindi anaishi kwa wazazi wa marehemu
Ila la muhimu waende mahakamani hao ndo waamuzi na watalaamu wa sheria, nazungumzia niliyowahi yaona
 
Hawezi pewa na hana haki sababu hajachuma na ila kuna sehemu ya watoto kingine mwambie aache tamaa
Tuwaachie wanasheria watupe tafsiri sahihi ya kisheria.hapa unaonekana umetumia hekima zako
 
Back
Top Bottom