Ndugu zangu ukisoma sheria ya mirathi kwa sheria ya mirathi ya Serikali, yaani Kwa mfano mume na mke walofunga ndoa ya kikristo, sio ya kiislam wala ya kimila. Mgao wa mali unakuwa hivi: mke wa marehemu anapewa 1/3 ( theluthi moja) ya mali. Watoto wanagaana kilichobaki kwa usawa bila kujali wa like au wa kiume. Sharti mke awe mke wa ndoa ya kikristo au ya Serikali. Mke anapewa bila kujali mchango wake kwenye hiyo mali.
Ninachokiona hapa watu mmechanganya kati ya mambo mawili, mgao wa mali wakati wa kuachana na mgao wa mali baada ya mwanandoa mmoja kufariki.
Naomba tuelewe kwamba hapa mtu aliyemuoa huyu mke aliyemuacha kwao na kwenda kuishi na mwanamke mwingine amefariki, pili ni mwanume alimtelekeza huyu mke kwao ( kwa kina mwanaume) na huyo mke alikaa huko kwa miaka mitatu ndipo mkwe wake na wanandugu wengine wakamruhusu arudi kwao maana mumewe kila akiitwa haji. Ndugu zangu hapa mama hakuvunja ndoa, kama binadamu ana haki ya kujamiiana, haki ya kuzaa watoto, na haki ya kutunzwa Kama mke ambazo zimeporwa na huyu mume. Bado kaachiwa watoto anatunza peke yake.Ili ndoa ya aina hii ivunjike inatakiwa taraka.
Sawali langu lilikuwa kutaka kujua ni Nani mwenye haki ya hiyo 1/3 kati ya hao watu wawili, huyo mwanmke aliyefunga ndoa na marehemu au huyu aliyekuwa akiishi nae? Kingine ndoa kama ni ya kikristo au ya kiserikali haitambui watoto wa nje ya ndoa hapa tunafanyaje maana huyu mama wa pili ana watoto 5 wa kwanza ana 3 msaada jamani huku mambo ni moto.