mcTobby
JF-Expert Member
- Feb 16, 2018
- 4,072
- 12,119
Kwema wadau na wanajamvi wote humu? natanguliza salamu.
Ni matamanio yangu kama mwanadamu tokea nikiwa mdogo kuingia kwenye hii career ya kurusha ndege. Nikasema anyway, nikimaliza chuo (nilimaliza mwaka jana B. Degree in Social Science), nikipata kazi nitadunduliza kidogo kidogo ndani ya hata miaka miwili nisomee hata leseni ya PPL (Private Pilot Picense) na CPL (Commercial Pilot Licence) hapo terminal one kwenye chuo cha Mosswood Dar es Salaam, ila my expectations kwa hali ya upepo ilivyo naona my dreams are faded away.
Hii inanipa sana stress muda mwingi. Nikiwaza ajira rasmi sina naishia kujilaumu na self guilt. Hapa nawaza kwa hivi vibarua vya kuunga unga vya shambani na ujenzi (japo ni za msimu) nijikusanye tu nisomee tu udereva lakini nikiangalia home na life lilivyo naona bado hali hairuhusu maana ndio inabidi nijitutumue kumpiga mother tafu(single mother) na wadogo zangu ambapo mmojawapo anatarajia kujiunga kidato cha tano muhula huu wa 2021/2022.
Nikisema niwatonye ndugu naona tu ni miyeyusho maana wengine hawakutaka niende hata chuo. Hivyo inabidi tu niugulie ndani kwa ndani tu labda kwa kujifariji tu inanibidi niwe naingia JF kusoma post za kina Mshana Jr ,ROBERT HERIEL na members wengine ili ku-gain tu chochote kwenye akili kama tiba ya stress.
KAMA WADAU WA MTANDAO WA JF,
Mnanishaurije mimi ndugu yenu maana mimi kama kijana sitaki ndoto zangu zife kizembe ilihali nina nguvu?
Nimeona kuwashirikisha humu ili nione lolote mtakaloniambia nichukue ushauri wenu (unaofaa pasipo kuvunja sheria).
Natanguliza shukurani zenu kwa dhati.