Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Nchi yetu tangu 1960 baada ya wakoloni kutuachia nchi yetu kulikuwa na vitu vinaitwa miiko!! Kulikuwa na tamaduni zetu na haki ya watu kuishi kulingana na tamaduni zao!! Seke seke la Wamasai Ngorongoro linasikitisha sana! Hata kama mnagogoro na wao ndio muondoe huduma za afya na madawa yasipelekwe? Hata kama ndio tunatafuta maendeleo au fedha za hisani ndio tuzibe masikio?
Wamasai wameomba kusikia angalau hata neno au tamko la utawala ndio kwanza naona vikosi vya FFU vinaingia mbugani na tangazo la kuvifuta kanisa vijiji vyote!! Wamasai ni sawa na samaki ameumbwa kwa asili ya kuishi majini huwezi kumtoa na kumpeleka nchi kavu ukidhani unamsaidia!! Mmeshindwa hata kukaa nao kuzungumza na kumaliza utata huu!! Mnadhani mkianza kuvimbishiana misuli mshindi atakuwa nani?
Watawala mmekuwa na jeuri na kiburi kilichopitiliza, sio tu kiburi na dharau pia!! Nyinyi mnawaona kama ni wachache lakini Tanzania nzima inaweza kusimamia nyuma yao na mambo yakawa magumu!? Usiudharau upele kwakuwa ni mdogo!! Unaweza kuondoa uhai wa mtu endapo utakuwa mkubwa.