Kuna kijana mmoja msomi hapa mtaani kwetu alipata fursa ya kwenda kufanya kazi kwenye kiwanda kimoja kikubwa nchini marekani, baada ya kufanya maandalizi ya kwenda safari yake alilazimika kufanyiwa vipimo vya afya ikiwemo HIV test.
Alipopimwa alikutwa Positive, ni takribani mwezi sasa tangu apime kijana huyo ambaye alikuwa ni handsome kwa muonekano wa mwili wake kwa sasa amekuwa zaidi ya babu kizee, amekonda amebaki mifupa na kutembea kwake kwa shida.
Nashindwa kuelewa ni kitu cha ghafla kilichompata kijana huyu mpaka kuwa na hali hiyo, anyway, na kwa niliyoyaona sitashawishika kupima Ukimwi bora tu niendelee kuishi kwa matumaini.
NB :Sishawishi wengine wasipime huo ni msimamo wangu tu.
Tupunguze uasharati jamani Ukimwi bado upo.
Sent using
Jamii Forums mobile app