Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 1,222
- 2,912
Mgomo wa mabasi ya abiria na maroli umeitikisa nchi. Umewaonyesha viongozi wa serikali kwamba nchi inaweza kusimama kwa muda na mambo yasiende wanavyotaka wao. Pongezi sana kwa ujasiri huu wa madereva
Hata hivyo, pamoja na pongezi hizi bado nina mashaka sana na usalama wa madereva wote waliogoma na usalama wa kazi zao
Mashaka yangu mimi kwa hawa madereva yanasababu kuu mbili:-
1. Mabosi wao ambao ndio wamiliki wa hayo magari ni wakwepaji wakubwa wa kulipa kodi za serikali na wana michezo mingi ya hatari lakini ya faida kwao wanaocheza na serikali
Swali ni dogo sana, serikali ikiwapa masharti ya kuwashughulikia madereva watapinga? Wana nguvu ya kusimama na madereva wao dhidi ya serikali hadi mwisho?
2. Viongozi wa juu wa madereva wenyewe wakitikiswa hawatatikisika? Hakuna machawa wa serikali watakao wageuka wenzao?
Kubwa zaidi mgomo huu umeifunua nguo ya ndani ya idara ya usalama wa Taifa na ule unyeti wake ukaonekana hadharani;
hebu fikiria nchi yetu ilivyokuwa kubwa,
jinsi tunavyoambiwa kuwa mkono wa serikali ni mkubwa;
kwamba watu wa idara ya kukusanya taarifa nyeti wako kila mahala;
lakini pamoja na unyeti na intelijensia makini ya watu wa idara nyeti,
bado madereva ambao wengi elimu yao ni ya wastani kiasi cha kuchukuliwa poa poa na baadhi ya makundi ya wasomi wameweza ku - organise mgomo nchi nzima kwa dakika chache tu watu tumeamka na kukuta kila stendi kubwa katika nchi hii hakuna basi linalosafiri.
Wamewezaje kujipanga kiasi hicho bila kugundulika?
Inavyoonyesha ni mkakati wa muda mrefu na kulikuwa na mawasiliano ya kujipanga kati yao, wamefanikishaje?