Kwa hali ya nchi ilivyo sasa; madereva waliogoma wajiandae kisaikolojia

Kwa hali ya nchi ilivyo sasa; madereva waliogoma wajiandae kisaikolojia

Nimewahi kuishi South Africa, Kuna siku nikiwa Cape town, nipo kwenye Tax (sisi huku tunaita Daladala) Tax imesimama kwenye Mataa, ni njia 4, njia zote hazikua na Magari muda huo, ilikua Tax yetu tu ikienda Mjini....!

Nikajisemea tunasubiri Taa zituruhusu wakati hakuna gari ingine, nikasema ingekua Bongo hapa, Dereva wa Dalala keshaondoka muda mrefu, vile nilikua siti ya mbele nikamuuliza Dereva wa Kirangirangi, Kwa Nini usipite tu coz hakuna Gari ingine na hakuna Traffic!

Akanambia ni kweli nchii hii Traffic ni wachache, wapo kwenye Road blocks ndiyo utawakuta Kwa Wingi, akasema barabara zote hizi Mjini hapa Zina Camera, akaanza kunionyesha Camera, akasema kule Control room Kuna Maafisa wa Traffic Kazi Yao ni kuangalia Magari yanayofanya Makosa, ukifanya kosa flani, wanaweka kwenye Record kosa ulilofanya, na Ushahidi wa Video, hata yakiwa Makosa 10 wata record, akasema kuna Magari yanajurikana Dereva ni nani, kama Daladala, Mabus makubwa n.k kesho tu wanakupigia simu kukupa taarifa ya Kosa ulilofanya na wanakutaka ukalipe fine, Kwa zile gari za kuazima basi watampigia simu Mmiliki, usipoenda kulipa Kwa wakati, siku ukienda Ku renew Leseni ama kulipa Bima ya Gari ama chochote utakutana na lundo la fine za kulipa zingine zikienda straight Kwa Dereva zingine Kwa Mmiliki coz yy ndiye anamjua Dereva, anasema kama Dereva ukishindwa kulipa, hupewi Leseni Yako mpaka ulipe, kama itachukua Mwaka kulipa ama miaka 2 ni sawa.

Anasema Camera zimewafanya wamekua na Nidhamu barabarani, sehemu yakusmama atasimama, sio ya ku overtake atakaa kwenye Mstari....!
Huku kwetu janjajanja nyingi na kufika huko sio kwamba hatuwezi ila kwasababu polisi wengi wanapenda kuwa traffic sababu hiyo hiyo inayowafanya polisi watamani kuwa matrafic ndio huchangia kukwamisha miundombinu kama hiyo

Bila mpokea rushwa hakuna mtoa rushwa, serikali ikiweza kudhibiti wapokea rushwa mambo mengi yatanyooka, sheria zitafuatwa na mapato ya serikali yataongezeka
 
Sidhani kama kuna mahali nimesema hoja zao sio za msingi, bali najaribu kujiuliza kama wana back up ya waajiri wao ili wanapopambania hizo haki zao isiishie kwa wengine kupata madhara na hatimaye kukosa msaada
Fuailia statement ya ABOA leo, wanawaunga mkono 100%
 
Back
Top Bottom