Kwa hapa africa kutatokea tena wanamuziki hawa wataalamu? Franco na oliver ngoma?

Kwa hapa africa kutatokea tena wanamuziki hawa wataalamu? Franco na oliver ngoma?

Franco Luambo wa tp jazzy,
aliwahi kuandika wimbo wa kumponda mobutu sesseko akatupwa ndani 😅. Baadaye tena akaimba wimbo wa kumsifia ndio alipoachiwa na urafiki ukadumu zaidi.
huyu jamaa alikuwa nyoko 👍
 
Wanamuziki kote duniani wanatengenezwa na mazingira, nyakati, mifumo ya kiutawala ya dunia pamoja na technology.

Nitakupa mfano, hakuta tokea tena wanamuziki kama Bob marley, culture, peter tosh n.k, sababu hali ya kisiasa duniani ndio iliwatengeneza fikra na kuwa wanamuziki wa kimapinduzi. Leo dunia imebadilika, hawawezi kuwepo wanamuziki wenye fikra za kupambania ukombozi wa muafrika.

Come to Franco, sio yeye tu, ila muziki wa Rumba ya congo asili sasa inapotea. Pop music imeingia kwa kasi huko congo. Sikiliza album wanazotoa new generation ya wacongo utakubaliana nami, mf Tokoos ya fally. Kimsingi hakuta tokea tena mithili ya Franco.
 
Franco Luambo wa tp jazzy,
aliwahi kuandika wimbo wa kumponda mobutu sesseko akatupwa ndani [emoji28]. Baadaye tena akaimba wimbo wa kumsifia ndio alipoachiwa na urafiki ukadumu zaidi.
huyu jamaa alikuwa nyoko [emoji106]
Huo wa kumponda unaitwaje
 
Wandugu japo mimi sio mhenga lakini huwa nina mtindo wa kusikiliza nyimbo za zamani hivyo nimeskiliza nyingi sana hata nilipowahi kuwa dj ujanani nilizipiga na mzee wangu anazo nyingi.
Sasa kwa upande wangu nauliza kutawahi kutokea tena wasanii wataalamu africa kama Franco na huyu wa majuzi kati kati wa kuitwa oliver ngoma?
Najua wapo wengi waliotisha na bado wamo akiwemo koffi olomide
Album zake tatu kati ya nne ni moto sana ukianza na Bane, Adia na Saga ...Seva haikua nzuri kama hizo pengine sababu ni kuwa hakufanya na producer wake wa siku zote Manu Lima RIP Oliver N’Goma a.k.a NOLI
 
Oliver N'goma alikuwa mkali pia
Uwe sehemu iliyotulia usikilize nyimbo kama

Alphonsine
Lili
Lusa
Bane
nk.

Burudani sana...Ukisikiliza album ya Bane huwezi kuruka nyimbo kuanzia Bane, Alphonsine, Icole,Lusa, Lili, Mayumba, Julie na Mugetu Gole. Vivyo hiyo kwenye album yake ya pili Adia
 
Muache utani na kiumbe anaitwa Oliver N'goma
Huyu mwamba ni mfalme wa Zouk
Aiseee vibao matata kama
Bane
Adia
Nge
Lili
Saga
Alphonsine
Mukuili
Ngebe
Noli
Lina
Seva
Melia
Julie
Barre
Betty
Mayumba
Na nyingine nyingi hakika Oliver N'goma sijaona mwanamziki wa kumfikia aisee huyu jamaa hakika aliufanya mziki wa zouk uwe na vionjo vitamu na miondoko adimu yenye radha ya kipekee kabisa
Roho hua inaniuma sana kumpoteza nguli huyu hakika wa Gabon,Afrika na dunia ilipoteza ladha adimu sana aisee
R.I.P Noli😢😢😢
 
Back
Top Bottom