Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu mnyonge mnyongeni lakini Haki Yake mpeni, Rais Samia Anastahili kupewa Haki yake, Haki ya kupongezwa, kuungwa Mkono, kupewa Faraja, kutiwa Moyo na kupewa ushirikiano.
Rais Samia Alipokea Nchi katika Kipindi Kigumu Sana kiuchumi, Alipokea Nchi kipindi Cha mlipuko wa ugonjwa wa CoVID 19, kipindi ambacho viwanda vingi vilikuwa vimefungwa ,vinafungwa au kupunguza wafanyakazi wake, Alipokea Nchi kipindi ambapo uchumi wa Dunia ulikuwa unatetemeka, kipindi ambacho ajira zilikuwa zinafungwa na kupungua, kipindi ambacho uzalishaji viwandani ulikuwa unapungua siku Hadi siku, kipindi ambacho wawekezaji walikuwa wanazidi kupungua kutokana na mtikisiko wa uchumi wa Dunia
Alipokea Nchi ambapo watu katika mataifa mbalimbali walikuwa wamejifungia ndani, kipindi ambacho kulikuwa na mfumuko wa Bei Duniani, Kabla haja kaa sawa Vita vya Ukrein vikaingia Kati, Hali iliyochochea uharibifu wa uchumi wa Dunia, mfumuko wa bei ukazidi kupaa zaidi ,Nishati ya mafuta ikawa haishikiki Wala kugusika, kila Kona ya Dunia ikawa Ni vilio na kelele za ugumu wa maisha na uchumi mbaya
Mama huyu na Rais huyu shupavu kabisa, Msikivu, Mzalendo, Imara, Mwenye Maono ya Mbali, Ndoto kubwa juu ya Tanzania mpya na Bora alianza kuusuka uchumi wetu uliokuwa umeharibiwa na CORONA pamoja na Vita vya Ukrein, alianza kuimarisha Diplomasia yetu ya uchumi, akafungua Ukurasa mpya wa kidiplomasia na majirani zetu, Afrika na Dunia nzima kwa ujumla.Taratibu tukaanza kuona mafuriko ya watalii na wawekezaji hasa baada ya wazo lake la kibunifu maarufu Kama royal Tour lililotangaza vivutio vyetu vya utalii na nchi yetu kwa ujumla.
Rais Samia akaimarisha secta binafsi ili iweze kukua vizuri na kutengeneza fursa za ajira kwa vijana, akazunguka huku na kule kuwashawishi wawekezaji katika secta tofauti tofauti, hatimaye wakaanza kuja nchini mwetu.
Akajitahidi kutoa ajira kwa vijana takribani elfu 42 katika secta karibia zote zikiongozwa na secta ya Elimu na Afya,
Rais Samia katikati ya mfumuko wa Bei akachukua hatua ya kukabiliana nao kwa kutoa Ruzuku katika Nishati ya mafuta pamoja na pembejeo za kilimo, Hali iliyopelekea kushuka kwa Bei sokoni na kutoa ahueni ya maisha kwa mtanzania, Hali ya kiuchumi imezidi kuwa njema na ya kuridhisha Sana, kwani Amejenga uchumi jumuishi unao mgusa kila mtanzania na kumnufaisha kila mtu kutokana na kuwekeza katika miradi inayogusa mtanzania mnyonge moja kwa moja, Hii ndio sababu ya Kuendelea kukubalika na kuungwa mkono na watanzania wote
Kila utakapokwenda unakuta Rais Samia anafanya kazi kubwa Sana, Unakuta umoja na upendo umetamalaki miongoni mwa watanzania, watanzania Wana amani kwa kuwa ameliunganisha Taifa na kuwa kitu kimoja ndio sababu hata viwanjani unaona picha zake zikitawala na kutamalaki huku watu wakishangilia kwa shangwe ,Vifijo na Nderemo
Watanzania Tuendelee kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa, Tuwe na Subira kwa Yale mambo yanayokuwa katika utekelezaji, tumwombee Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia watanzania, Rais Samia Ni zawadi kwetu watanzania tunayopaswa kujivunia kwa kipindi hiki, Nafikiri mmesikia kwingineko badala ya kujadili maendeleo wameanza kujadili habari za kuongeza miaka ya Rais kukaa muda mrefu Zaid madarakani. Watanzania tuna bahati kwa kuwa Rais wetu muda wote anajadili habari za maendeleo tu na namna ya kumkwamua kiuchumi mwananchi mnyonge
Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti
Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627( Kwa maoni juu ya ujenzi wa Taifa letu