Kwa Hapa Tanzania, ukikosa kazi kabisa sio lazima ukabebe tofali au kazi za ujenzi, Nenda kijijini kalime.

Kwa Hapa Tanzania, ukikosa kazi kabisa sio lazima ukabebe tofali au kazi za ujenzi, Nenda kijijini kalime.

Brojust

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2016
Posts
349
Reaction score
1,024
Mwanangu mpambanaji, umekosa mtaji, mjini hakueleweki, ushamaliza degree yako na home hapaeleweki kazi hazieleweki.

Sikia, chukuwa vyeti vyako, scan, tunza kwenye email yako, tengeneza template ya barua ambayo unaweza ku edit hata kwa simu.

Piga simu kujijini kwenu, haswa kwa watu wa mbeya, iringa, morogoro, bukoba, na mikoa yote ya kilimo

Weka kisomo chako pembeni, andaa ndugu zako nenda zako kalime, Kaa miaka 3 then njoo town fungua duka la jumla.

Kama una roho mbaya tafuta mwanamke asiye na kazi ila asiwe mjuaji zaa nae muoe muweke dukani.

Chukua boda boda (hapa inabidi uwe na akili timamu, kama na wewe ni chenga utakufa mapema sana) ingia barabarani.

Ukikaa miaka 5 mpaka 6. Tayari una kiwanja, watoto wanasoma, mke unae, ujenzi unaendelea. Vile vyeti ulivyoweka kwenye pdf achana navyo piga kazi.

Risk kubwa ya mambo haya ni ROHO MBAYA. Anza hii mapema sana January 2025.

NB: Kumbuka ukishajipata, usiache kula kitimoto rosti na kilimanjaro mbili tu. (Zingatia neno mbili tu)

Nawasilisha.
 
Mkuu hivi unajua kwamba ukulima nao unahitaji mtaji WA kutosha tu au umekurupuka Tu na kuanza kuandika andika?

Kwanza umejuaje kama kila mtu ana shamba kwao?
Wewe acha kukatisha watu tamaa, kwenye kilimo kuna maruzuku kibao ni kitafuta ndugu zako tu walio kijijini na wanaotegemea kilimo, sikia kukaa mjini na kubeba tofali au fundi msaidizi na kwenda kulima kipi bora. Kumbuka happy una degree ya business administration na Huna fani yoyote hata udereva.
 
Isije ikawa unasukumwa na kibri.......
 
Mentality iliyojengeka ni mjini kuna kazi kuliko kijijini. Kazi za vijijini ni msoto tu hazina kipato. Watu walisoma ili wakapate kazi nzuri mijini. Hii dhana imepitwa na wakati, kijijini sasa hivi ukilima utapata hela za mishahara ya mwaka mzima ya mtumishi fulani wa umma. Kilimo kimekuwa na tija sana miaka hii mazao yanahitajika sana sokoni. Soko la mazao limekuwa kubwa sana na wazalishaji ni wachache
 
Kwanza kuna watanzania wengi ambao hawana mashamba waliyorithishwa kwa sababu mbalimbali. Na hata kama una hilo shamba kama huna mtaji hicho kilimo huwezi kufanikiwa.

Kilimo kinahitaji muda, mtaji, ufuatiliaji na uvumilivu huwezi kufanikiwa kama kilimo cha PDF kirahisi hivyo.
 
Ni heri kuingia huko polepole/kidogokidogo kuliko kukaa mjini bila shughuli ya kueleweka. Pia kijana akijipanga akaondoa aibu akaingia kwenye ufugaji mdogo mdogo (kuku, bata au mbuzi), baada ya miaka 5 anakuwa na kipato cha maana.
Kwa hali ilivyo na inavyoenda, panahitajika kujitoa mhanga
 
Suala ni kujichanganya na kila shughuli halali itakayokupatia riziki. Na mambo ya ufugaji huu ushauri unawafaa wale wenye kwao au wale walau sehemu wanazoishi kuna eneo lenye nafasi lakuweza kuendesha shughuli hizo.
 
Wewe acha kukatisha watu tamaa, kwenye kilimo kuna maruzuku kibao ni kitafuta ndugu zako tu walio kijijini na wanaotegemea kilimo, sikia kukaa mjini na kubeba tofali au fundi msaidizi na kwenda kulima kipi bora. Kumbuka happy una degree ya business administration na Huna fani yoyote hata udereva.
Tatizo lako wewe unaassume kila mtu ana ndugu kijijini ama ana shamba amerithi kutoka kwa wazazi wake.

Kuna watu wanaishi vijijini katika kiwanja kidogo Sana na kote wamejenga nyumba na choo hata pa kupanda mboga Tu hawana.

Hata huo ukulima nao unahitaji mtaji WA kutosha wa kutayarisha shamba,kununua pembejeo,palizi na kadhalika
 
Back
Top Bottom