Kwa haya anayoyafanya Samia kijijini Kizimkazi hayana tofauti na aliyokuwa akifanya Magufuli Chato

Kwa haya anayoyafanya Samia kijijini Kizimkazi hayana tofauti na aliyokuwa akifanya Magufuli Chato

Doslamari

New Member
Joined
Jun 21, 2024
Posts
4
Reaction score
1,499
Kwanza yeye ni Rais wa JMT kila mara yuko Zanzibar kuzindua miradi. Kijiji kidogo hicho mapesa yote ndani ya miaka 3 hela ililipelekwa pale ni nyingi sana. Hii ni kwanza ni aibu na kashfa kwa Rais wa nchi nzima.

Tabia hii alianza Magufuli, kabla ya hapo huu ubaguzi usio na haya haukuwepo. Tanzania mikoa yetu ni masikini bado, havina viwanja unaenda kujenga uwanja mkubwa namna ile kijijini bila hata haya? Hii ni dharau na asije akawa Rais wa kuja kuuvunja huu muungano.

Tunaona Zanzibar uwekezaji uliofanyika ndani ya hii miaka 3 ni shule za maghorofa, haya yanaweza kuwa maandalizi ya kuuvunja muungano. Hii ni miaka 3, je, vipi miaka 6 iliyobaki?

Nenda mkoa wa Manyara pale Mbulu kuna uwanja umetelekezwa, wambulu ndio waliiletea nchi hii sifa katika olympic lakini sahivi wametelekezwa. Nchi inakoelekea itakatwa vipande vipande.

Kuanzia awamu ya 5 ni nchi ya ubaguzi kuanzia Waziri Mkuu. Eti NMB, CRDB ndio imejenga, hayo mabenki yalikuwepo miaka mingi kwa nini sasa? Viongozi wa sasa hivi ni janga la Taifa, hivi nchi ikigawanyika wataeneo na kupona ndani ya hivyo vijiji vyao?
 
Ameamua kukopi na kupesti vyote vya JPM

Usishangae atakayekuja baada ya Samia, naye akafanya hayo hayo🙌

Nchi iliyokosa maono
 
Mulimchekea yule marehemu mama anacheza na style hiyo hiyo kweli kiz mkazi inaenda kuwa New york city.
Dawa ya haya yote ni katiba mpya
 
Kwa ujinga huu, siku mmasai akipata urais, Ngorongoro creator patageuka kuwa city centre
 
Samia:Kizimkazi Sports City.
Magufuli: Chato City and Man made Burigi National park.
Mobutu Sese Seko.Gbadolite, Paradise in the Jungle!

Kuna mwingine alijenga "Saint Peters Basilica" kijijini kwao ya kusalisha watu 600 badala yake hata waumini 100 walikuwa hawatimii.
 
Back
Top Bottom